Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dk Hussein Kidanto (kushoto)
akimtambulisha Kaimu Mkurugenzi mpya wa Hospitali hiyo, Profesa Lawrence
Mseru (kulia) ambaye ameteuliwa jana na Rais John Pombe Magufuli. Jana
Rais Magufuli amemuamishia Dk Kidanto katika Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii.
Kaimu Mkurugenzi mpya wa
Hospitali hiyo, Profesa Lawrence Mseru ambaye ameteuliwa jana na Rais
John Pombe Magufuli akizungumza na menejimenti ya hospitali hiyo jana.
Baadhi ya wakurugenzi wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi mpya wa Hospitali hiyo Profesa Lawrence Mseru.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
ya Umma (MNH), Aminiel Aligaesha (kushoto) na mwanasheria wa hospitali
hiyo, Veronica wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi mpya wa Hospitali hiyo
Profesa Lawrence Mseru.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru leo ameanza
kazi na kuwataka wafanyakazi wa hospitali hiyo kuwahi kazini kwa wakati
na kufanya kazi kwa bidii.
Profesa Mseru ametoa kauli hiyo
leo jijini Dar es salaam baada ya kukutana na menejimenti ya hospitali
hiyo ambayo inajumuisha Wakurugenzi 14. Mkurugenzi huyo amekutana na
menejimenti hiyo majira ya saa 6:00 mchana katika ukumbi wa mikutano wa
hospitali hiyo.
Pia, amekutana na kamati
tendaji ya hospitali , wakurugenzi, wakuu wa idara, mameneja wa majengo
ikihusisha Sewahaji, Mwaisela, jengo la watoto na jengo la wazazi saa 8:
00 mchana.
Pamoja na mambo mengine katika
kikao hicho, wakurugenzi wameeleza mafanikio na changamoto mbalimbali
zinazoikabili hospitali hiyo.
Profesa Mseru ameteuliwa jana
kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo baada ya Dk. Hussein
Kidanto kuhamishiwa wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa ajili ya
kupangiwa kazi nyingine.
EmoticonEmoticon