Watumishi wa Wizara ya
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo wakifurahia jambo wakati wa hafla ya
kumuaga aliyekuwa katibu mkuu wa wizara iyo Bi Sihaba Nkinga ambaye
amehamishiwa wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto.Pia
aliyekuwa naibu katibu mkuu wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel
ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara hiyo na Mwamini juma Mwalemi
ameteuliwa kuwa Naibu Katibu mkuu wa Wizara hiyo.
Naibu Katibu Mkuu mteule Wizara
ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Bi Mwamini juma Mwalemi
akizungumza na watumishi wa wizara hiyo leo hii jijini dar es
Salaam.Kulia kwake wa kwanza ni Katibu Mkuu mteule wa Wizara iyo Prof
Elisante Ole Gabriel na wa mwisho ni Bi Sihaba Nkinga ambaye alikuwa
katibu mkuu wizarani hapo na ameteuliwa kuwa katibu mkuu Maendeleo ya
Jamii,Jinsia na Watoto.
Mkurugenzi msaidizi Lugha,Idara
ya Utamaduni kutoka Wizara ya habari,vijana,Utamaduni na Michezo akiimba
Tenzi kwa ajili ya Kumuaga aliyekuwa katibu mkuu wa wizara hiyo bi
Sihaba Nkinga leo jijini Dar es Salaam.
Katibu mtendaji Bodi ya filamu na
michezo ya Kuigiza kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo
akimkabidhi zawadi ya filamu za kitanzania aliyekuwa katibu mkuu wa
wizara hiyo Bi Sihaba Nkinga wakati wa sherehe za kumuaga leo jijini Dar
es Salaam.
Wakuu wa Taasisi
mbalimbali za Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni zikijumuisha
MichezoTasuba,Basata,bakita,TBC na BMT wakiwa
katika picha ya pamoja na viongozi wapya wa wizara hiyo na katibu mkuu
anayehama wizara Bi Sihaba Nkinga.(katikati).
EmoticonEmoticon