RATCO YALITIKISA JIJI LA TANGA IKISHUSHA MABASI MAPYA,YATANGAZA SAFARI ZA USIKU IKIWEMO RUTI MPYA YA TANGA-ARUSHA

December 19, 2024



 





Na Oscar Assenga, TANGA

KAMPUNI y Mabasi ya Ratco ya Jijini Tanga imenunua mabasi mapya mawili na kuyaingiza Jijini Tanga huku wakitangaza mpango wa kuanzisha ruti mpya ya mikoa ya Kanda ya Kaskazini pamoja na safari za usiku.

Akizungumza wakati wa mapokezi ya mabasi hayo yaliyoanzia kwenye eneo la Kwaminchi Jijini Tanga, Meneja Rasilimali Watu na Afisa Mahusiano na Mawasiliano wa Kampuni ya Ratco Hassani Hashim alisema kwamba wameongeza ili kukidhi mahitaji ya wateja wao.

Alisema pia kuondoa adha ambayo wanapata abiria wao na wao wameamua kuongeza ruti na mabasi mapya yenye hadhi ya VIP tofauti na ilivyo katika makampuni mengine nchini 

Alisema pamoja na hilo lakini wataanza safari za usiku hivi karibuni ili kuwezesha abiria wanaosafiri usiku kuweza kusafiri lengo likiwa ni kuwapa wananchi na wateja wake kile ambacho wanakitaka.

Akizungumza namna walivyojipanga kwenye msimu huu wa sikukuu alisema katika kipindi hicho kumekuwa na migigoro mingi na kuibuka matepeli ambao wanawalangua tiketi wananchi hivyo kwa kuliona hilo wamekuwa wakikata tiketi kwa njia ya mtandao ili kuwaepusha wananchi na adha hiyo.

 Hashim alisema mfumo waliokuwa nao ni wa kisasa zaidi kwani unamuwezesha abiria kukata tiketi akiwa nyumbani kwake bila kufika ofisini kwao na hivyo kuendelea kufanya shughuli zao huku wakiwa na uhakika wa safari.

 “Leo tumepokea gari mpya huu ni muendelezo wa kupokea gari nyengine mpya mwaka 2025 na tumedhamiria kuhakikisha tunatoa huduma nzuri na zenye viwango vya hali ya juu ili kuendelea kuwa kwenye kiwango chetu cha ubora siku zote”Alisema

 Awali akizungumza wakati wa mapokezi ya mabasi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabasi ya Ratco Mohamed Salim “Ratco”alisema kwamba wamejipanga vizuri kutoka huduma bora na zenye viwango na hawaogopi ushindani kutokana na kwamba ndio unawapa chachu ya kuwafanya wasijisahau na kujipanga zaidi na zaidi.

 “Kikubwa ni kuongeza huduma na kuendelela kuwa katika kiwango na ubora wao waliokuwa nao siku zote na tunawakaribisha kampuni yoyote inajisikia kufanya biashara Tanga hivyo waleta uhsindani “Alisema

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »