MALINZI AMSHUKURU TENGA
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amemshukuru Rais wa
CECAFA, Leodgar Tenga kwa kuipa Tanzania uenyeji wa mashindano ya Vilabu Bingwa
Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup) iliyomalizika jana kwa klabu ya Azam FC
kutawazwa Mabingwa wapya wa michuano hiyo.
Aidha
Malinzi ameishukuru Kamati ya Ndani ya Uendeshaji ya Michuano hiyo (LOC) kwa
kazi nzuri waliyoifanya ya kuandaa na kuhakikisha michuano hiyo inafanyika na
kumalizika katika hali ya usalama na amani.
Malinzi
pia amewapongeza wapenzi, washabiki na wadau wa soka nchini waliojitokeza
kushuhudia michezo ya michuano hiyo na kuonyesha nidhamu ya hali ya juu ndani
nan je ya uwanja kipindi chote cha michuano.
Rais
Malinzi ameipongeza klabu ya Azam FC kwa kutwaa Ubingwa Kagame, kwa kutwaa
ubingwa huo imeweza kuweka historia ya kutwaa Ubingwa huo kwa mara ya kwanza
tangu kuanzishwa kwake na pia kuwa klabu iliyocheza michuano hiyo na kuwa
Bingwa bila kuruhusu nyavu zake kutikisika.
Pia
Malinzi amewashukuru waandishi wa habari/vyombo vya habari kwa sapoti yao
wakati wa michuano hiyo. Shukrani hizo pia zimepelekwa kwa klabu za Yanga SC,
KMKM kwa kushiriki mashindano hayo.
U-15
YAREJEA KUTOKA ZANZIBAR
Kikosi
cha timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U-15), kimerejea leo
asubuhi kutokea kisiwani Zanzibar kilipokwenda kucheza michezo ya kujipima
nguvu na kombani ya U-15 ya kisiwani humo.
Katika
michezo miwili iliyocheza kisiwani humo, iliweza kushinda michezo yote miwili,
(4-0 ), (1-0), huku kocha Bakari Shime akiwapongeza vijana wake na kusema
wanaendelea kuimarika kuelekea kujiandaa
na kuwania kufuzu kwa fianali za Mataifa Afrika chini ya miaka 17
mwakani.
Baada
ya kurejea jijini Dar es salaam leo, kambi ya timu hiyo imevunjwa na vijana hao
watakutana tena mwisho wa mwezi wa Agosti kama ilivyo katika program yao ya
kukutana kila mwisho wa mwezi na kucheza michezo ya kirafiki.
Mwishoni
mwa mwezi Agosti timu hiyo ya vijana inatarajiwa kuelekea mkoani Tanga kucheza
michezo ya kirafiki na kombani ya mkoani humo, ambapo kocha wake Shime pia
anatumia nafasi hiyo kutazama wachezaji wengine wenye uwezo mzuri katika timu
za kombaini za mikoa kwa ajli ya kuwaongeza katika kikosi chake.
Mpaka
sasa timu hiyo ya vijana chini ya miaka 15 (U15) imeshafanya ziara na kucheza
michezo katika miji ya Mbeya na kisiwani Zanzibar.
IMETOLEWA
NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
-
Best Regards,
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
T: +255 22-2861815 I F: +255 22-2861815 I C: +255 713 455970
E: b.kizuguto@tff.or.tz, I W: www.tff.or.tz
A:I P.O.BOX 1574 Karume Memorial Stadium /Shaurimoyo/Uhuru Street I Dar es salaam I Tanzania
EmoticonEmoticon