Vikosi mbali mbali ya Majeshi vikiwa vimejipanga tayari kwa kungia uwanjani kwa ajili ya ufunguzi wa michezo ya majeshi 2015.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Songea Prof.
Nomarn Sigalla King akisalimiana na wachezaji wa timu ya jeshi kutoka
Mtwara.
.........................................
Na Amon Mtega ,SONGEA
MICHEZO
ya majeshi inayoshirikisha vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama
briged ya kanda ya kusini imefunguliwa rasmi na kaimu mkuu wa mkoa wa
Ruvuma ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Songea ,Pr Noman sigaa King huku
benki ya NMB tawi la Songea likiwa limetoa msaada wa jezi za mpira wa
miguu seti saba ambazo zenye thamani ya shilingi 3,000,000.
Akiongea
kwenye ufunguzi huo uliyofanyika leo katika uwanja wa michezo wa
majimaji uliyopo Songea ,Sigara alisema kuwa michezo hiyo itaimarisha
mahusiano ya kiulinzi baina ya mipaka yetu ya Tanzania kwa kuwa vyombo
vyote vya ulinzi na usalama vitakuwa na ushirikiano.
Alisema
kuwa ulinzi wa Tanzania katika mipaka yetu hautegemei jeshi moja tuu
bali ni ushirikiano wa vikosi vya majeshi mbalimbali kama vikosi hivi
ambavyo vimeshirikishwa kwenye michezo hii iliyozinduliwa na ambayo
itarajiwa kufanyika kwa wiki mbili.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Prof. Norman Sigalla King akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya The Might Elephant .
Aidha
Pr, Noman alizitaka taasisi za kifedha zilizopo hapa nchini kuwamstari
wa mbele katika kudumisha mahusiano ya mambo mbalimbali ikiwemo ya
michezo kwa kuwatoa misaada kama ilivyo kwa benki ya NMB.
“Taasisi
za kifedha zinauwezo mkubwa wa kutoa misaada ya ushirikiano kwa kuwa
zimekuwa na frunsa nyingi katika kufanikisha mahitaji yanayotakiwa na
wahitaji “alisema Noman Sigara ambaye ni kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma.
Kwa
upande wake kamanda Briged ya Tembo kanda ya kusini John Chacha awali
kabla ya uzinduzi huo alisema kuwa licha ya kufanyika kwa michezo ya
mpira wa miguu pamoja na mpira wa pete na wa kikapu toka kwenye vikosi
mbalimbali vinavyoshiriki alisema kuwa kutakuwemo na mchezo wa kulenga
shabaha ambao alidai kuwa ni mhimu kwa upande wa jeshi hilo.
Chacha
alisema kuwa mchezo wa ulengaji shabaa ni mchezo mhimu sana kwa jeshi
kwa kuwa ndio unaomfanya mwanajeshi kuwa tayari mda wote katika utendaji
wao wa kazi ambao huendana na shughuli hizo.
Kaimu Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Prof. Norman Sigalla King akionyesha ufundi wake wa
kumiliki mpira katika ufunguzi wa michezo ya majeshi.
Kwa
upande wake meneja wa benki ya NMB tawi la Songea Rehema Nasib
akikabidhi msaada huo wa jezi alisema kuwa benki hiyo imejijengea
utaratibu wa kuungana na jamii katika kutekeleza mambo mbalimbali ambayo
yanayo hitajika.
Rehema
alisema kuwa licha ya benki hiyo kujijengea tabia hiyo lakini bado
imekuwa ikithamini michango inoayotolewa na jamii pamoja na jeshi kwa
kuwa wamekuwa wateja wakubwa ndani ya benki hiyo.
Katika michezo hiyo zaida ya vikosi tisa vinashiriki michezo hiyo na tayari imeshaanza kuchezwa katika uwanja wa maji maji.
Baadhi ya washiriki wakifatilia mchezo
Katoka
kulia kwako wa pili ni Katibu wa SUFA akifatilia mashindano ya majeshi
na wa kwanza kulia kwako ni mtangazaji wa Jogoo FM Bw. Onesmo Emilani.
EmoticonEmoticon