Mtama
ukiwa umestawi vizuri katika moja ya shamba, hivi leo Kampuni ya
mawasiliano ya Vodafone imezindua mpango maalumu wa kuboresha maisha
ya wakulima wadogo wa Kilimo Klub utakaoanza kutekelezwa Tanzania.Nchi
zingine zitakazotekeza mpango huu ni Kenya,Ghana na India mpango wa
Vodafone Farmers Club unalenga kuboresha maisha ya wakulima wadogo wenye
kujishughulisha na kilimo ili kuwaongezea uzalishaji kupitia kisaidizi
maalumu ambacho ni simu za mkononi.
Zabibu
zikiwa zimestawi vizuri katika moja ya shamba Dodoma vijijini kufuatia
kilimo bora na cha kisasa,kilimo hichi kinaongezewa nguvu na kampuni ya
Vodafone ambapo leo imezindua mpango maalumu wa kuboresha maisha ya
wakulima wadogo kama hawa wa Kilimo Klub utakaoanza kutekelezwa
Tanzania.Nchi zingine zitakazotekeleza mpango huu ni Kenya,Ghana na
India mpango wa Vodafone Kilimo Klub unalenga kuboresha maisha ya
wakulima wadogo kwa kuwaongezea uzalishaji kupitia kisaidizi maalumu
ambacho ni simu za mkononi.
Mfanyabiashara
wa soko la Mgandini Tanga,Hamis Mtote, akipanga mihogo aina ya
Kibandameno ambayo inatoka katika shamba la mfano lililoko Tarafa ya
Maramba Wilayani Mkinga ambapo Kampuni ya mawasiliano ya Vodafone leo
imezindua mpango maalumu wa kuboresha maisha ya wakulima wadogo wa
Kilimo Klub utakaoanza kutekelezwa Tanzania. Nchi zingine
zitakazotekeleza mpango huu ni Kenya,Ghana na India mpango wa Vodafone
Kilimo Klub unalenga kuboresha maisha ya wakulima wadogo kwa kuwaongezea
uzalishaji kupitia kisaidizi maalumu ambacho ni simu za mkononi.
Mfanyabiashara
wa soko la Mgandini Tanga, Salim Hamis, akipanga mihogo aina ya
Kibandameno ambayo inatoka katika shamba la mfano lililoko Tarafa ya
Maramba Wilayani Mkinga. Leo hii Kampuni ya mawasiliano ya Vodafone
imezindua mpango maalumu wa kuboresha maisha ya wakulima wadogo kama
hawa wa Kilimo Klub utakaoanza kutekelezwa Tanzania. Nchi zingine
zitakazotekeleza mpango huu ni Kenya,Ghana na India mpango wa Vodafone
Kilimo Klub unalenga kuboresha maisha ya wakulima wadogo kwa kuwaongezea
uzalishaji kupitia kisaidizi maalumu ambacho ni simu za mkononi.
Juma
Zombezi ambaye ni Mfanyabiashara wa soko la Mgandini Tanga,akiweka
mihogo yake kwenye mfuko tayari kwa kuuza hivi karibuni leo hii kampuni
ya Vodafone imezindua mpango maalumu wa kuboresha maisha ya wakulima
wadogo kama hawa wa Kilimo Klub utakaoanza kutekelezwa Tanzania. Nchi
zingine zitakazotekeleza mpango huu ni Kenya,Ghana na India mpango wa
Vodafone Kilimo Klub unalenga kuboresha maisha ya wakulima wadogo kwa
kuwaongezea uzalishaji kupitia kisaidizi maalumu ambacho ni simu za
mkononi.
Shamba
hili zuri la Mradi wa Kilimo cha Tangawizi linalimwa na kikundi cha
ujasiriamali cha ushindi kilichopo katika kijiji cha Mkongotema kata ya
Mkongotema tarafa ya Madaba Halmashauri ya Songea,Vikundi kama hivi
vinahitaji kupatiwa huduma bora za kuendeleza kilimo ambapo leo hii
Kampuni ya mawasiliano ya Vodafone imezindua mpango maalumu wa
kuboresha maisha ya wakulima wadogo wa Kilimo Klub kama hawa utakaoanza
kutekelezwa Tanzania. Nchi zingine zitakazotekeleza mpango huu ni
Kenya,Ghana na India mpango wa Vodafone Kilimo Klub unalenga kuboresha
maisha ya wakulima wadogo kwa kuwaongezea uzalishaji kupitia kisaidizi
maalumu ambacho ni simu za mkononi.
Kampuni
ya mawasiliano ya Vodafone leo imezindua mpango maalumu wa kuboresha
maisha ya wakulima wadogo wa Kilimo Klub utakaoanza kutekelezwa
Tanzania.Nchi zingine zitakazotekeleza mpango huu ni Kenya,Ghana na
India.
Mpango
wa Vodafone Kilimo Klub unalenga kuboresha maisha ya wakulima wadogo
kwa kuwaongezea uzalishaji kupitia kisaidizi maalumu ambacho ni simu za
mkononi.Mpango huu kwa mara kwa kwanza ulizinduliwa nchini Uturuki mwaka
2009.Asilimia 25 ya wakazi wa nchi hiyo ni wakulima na kupitia mpango
huu zaidi ya wakulima milioni 1.2 wamenufaika kwa uzalishaji wa mazao
kuongeka ambako kunaendana sambamba na ongezeko la kipato chao.
Kilimo
Klub itatekelezwa kwenye nchi husika kulingana na mahitaji ya wakulima
yaliyopo kwenye nchi hizo ila italenga kutumia simu za mkononi
kuwarahishia wakulima wadogo maisha kwa kuwapatia taarifa za masoko,hali
ya hewa,na huduma za kifedha.Mpango huu pia utatekeezwa katika nchi ya
New Zealand ambayo licha ya kwamba imepiga hatua kubwa katika sekta ya
kilimo lakini utalenga zaidi kuwakomboa wakulima wadogo nchini humo
kuongeza uzalishaji.
Mtendaji
Mkuu wa Vodafone anayesimamia kanda za Afrika,Mashariki ya Kati na Asia
Serpil Timuray amesema : “Moja ya tatu ya watu duniani wanategemea
kupata chakula kilichozalishwa na wakulima wadogowadogo wenye vipande
vidogo vya ardhi visivyozidi hekari 2.Teknolojia ya simu za mkononi
ikutumika ipasavyo inaweza kubadilisha maisha ya wakulima hawa yakawa
bora kutokana na ongezeko la uzalishaji utakaowezesha pato lao
kuongezeka.Kilichotokea nchini Uturuki kupitia teknolojia ya simu za
mkononi kubadilisha maisha ya wakulima ni ushahidi tosha kuwa Kilimo
Klub ni ukombozi kwa wakulima.
Serpil
Timuray aliongeza kusema: “Kwa kadri idadi ya watu inavyozidi
kuongezeka kuna haja ya kuangalia jinsi ya kuongeza uzalishaji wa
chakula kwa kuzingatia njia bora za matumizi ya ardhi.Mpango kama Kilimo
Klub wa Vodafone ni mzuri na una msaada mkubwa kuboresha maisha ya
wakulima na kuhakikisha kunakuwepo na chakula cha kutosha.
Uzinduzi
wa mpango wa Kilimo Klub wa Vodafone kwenye nchi 4 leo umekwenda
sambamba na uzinduzi wa sinema inayoonyesha huduma sita zilizopo chini
ya mpango huu zilivyoweza kuboresha kipato cha wakulima 70 milioni
nchini India kwa kuwawezesha kujipatia kipato cha dola za Kimarekani
bilioni 9 kwa mwaka.Familia nyingi za wakulima wa India zinaishi kwa
wastani wa matumizi yasiyozidi dola 4 za Kimarekani kwa siku.
Kwa
mujibu wa ripoti ya Connect Farming ya India iliyochapishwa na Vodafone
leo imeonyesha jinsi wakulima wengi walivyonufaika kupitia huduma
zipatazo 6 zinazotolewa kwao kupitia simu zao za mkononi na kufanikisha
kipato cha wakulima 70 milioni nchini India kwa kuwawezesha kujipatia
kipato cha dola za Kimarekani bilioni 9 kwa mwaka.
Ripoti
hiyo iliyofanywa na taasisi ya Accenture Strategy kwa ufadhili wa
Vodafone Foundation imebainisha kuwa matumizi ya simu kurahisisha kilimo
kumewezesha wakulima nchini India mapato yao kupanda kufikia wastani wa
dola Marekani 128 kwa mwaka kwa zaidi ya nusu ya wakulima nchini humo
tofauti na pato la dola ambapo hata hivyo bado kuna wakulima wengi
wanaoishi kwa chini ya dola 4 kwa siku wakiwa wanakabiliwa na changamoto
ya kupata chakula cha kutosha na kusomesha watoto.
Kwenye
ripoti hiyo imebainishwa kuwa nchi ya India ni moja ya nchi
inayozalisha chakula kwa wingi duniani ikiwa na wakulima wapatao
milioni 200 na karibu nusu yao wakifanya kazi kama vibarua kwenye
mashamba na asilimia 62 ya wakulima nchini humo wakiwa wanamilik
mashamba madogo yasiyofikia hekari 1 huku wakiwa wanakabiliwa na
changamoto za kupata taarifa za masoko,mbinu bora za kilimo cha kisasa
na taarifa zinginezo kama vile hali ya hewa.
Vodafone
na Accenture Strategy zimebuni nyenzo sita za kubadilisha maisha ya
wakulima nchini India kuwa murua kupitia simu za mkononi ambazo ni
kutoa huduma zifuatazo:
-Kutoa
taarifa za kilimo-Huduma hii inatoa taarifa za hali ya hewa,matukio
mbalimbali kama vile ni msimu gani wa kupanda mazao na kuvuna.Huduma hii
itawaongezea karibu wakulima milioni 60 nchini India kipato cha
wastani wa Dola za Kimarekani 89 ifikapo mwaka 2020.
-Kutoa
risti-Huduma hii inawawezesha wakulima kupunguziwa adha ya kupunjwa
wanapouza mazao yao na pembejeo za kilimo kwa kuwa inadumisha uwazi
katika masuala ya malipo na kuondoa udanganyifu.
-Kufanya
malipo na kupata mikopo-Kuwawezesha wakulima kutafuta huduma mbalimbali
za kuwarahishia kazi yao na kufanya malipo kutumia simu zao kama vile
huduma ya Vodafone ya M-Pesa,ilizinduliwa nchini India mwaka 2013 na kwa
muda mfupi imeonyesha mafanikio makubwa ya kufanya malipo na hadi
kufikia mwaka 2020 itakuwa imewanufaisha wakulima kwa kiasi cha Dola za
Kimarekani 690 kwa mwaka ambapo itawaongezea wakulima wastani wa
asilimia 39 mapato.
-Ukaguzi
na utunzaji nyaraka za kumbukumbu-Mpango huu unawezesha wakaguzi
kupitia kumbukumbu za wakulima kupitia njia ya kieletronikali kupitia
data za simu na inasaidia kuboresha ufanisi wa kazi za wakulima na
umeweza kuwaongezea baadhi ya wakulima pato kufikia dola za Kimarekani
612.
-
Kujenga mtandao bora wa uuzaji mazao- Mpago huu unawezesha wakulima
unawawezesha wakulima kuuza mazao yao kwenye vyama vya ushirika kwenye
maeneo na kubadilishana taarfa na kulipwa kutma njia ya simu. Njia hii
itawezesha hadi kufikia mwaka 2020 itaweza kuongeza pato la wakulima
kufikia dola za Kimarekani 271 na imeongeza mapato ya wakulima wengi kwa
asilimia 50 kwa sasa.
-Kuwezesha
upatikanaji wa simu zinazotumia internet (Smartphone)-Simu hizi ni
rahisi kuwezesha wakulima kupata taarifa japokuwaa bao ni za gharama
kubwa kwa wakulima wengi vijijini kumudu kuzinunua ingawa kadri ya
siku zinavyosonga mbele zinazidi kushuka bei.Hadi kufikia mwaka 2020
simu hizi zikitumiwa ipasavyo zaidi ya wakulima milioni 4 pato lao
litaongezeka hai kikia Dola za Kimarekani 675.
EmoticonEmoticon