Na Tinah Reuben, Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara Dar es salaam (JWT), Philimon Chonde
amesema suala la kupandishwa kwa kodi kwa asilimia mia moja limepitishwa
kinyemela bila ya wao kuwashirikisha wala kujadiliana na
wafanyabiashara hao.
Akizungumza
leo katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Lamada Hotel jijini Dar
es Salaam ukiwashirikisha wabunge, ameeleza kuwa mfumo wa kodi uliopo
umekaa kikoloni kwani unawakandamiza wafanyabiashara ili waendelee kuwa
tawala kwani haungalii uwiano uliopo baina ya wafanyabiashara wakubwa na
wafanyabishara wadogo.
Chonde
amesema kutokana na kuwepo kwa usumbufu wa kudai leseni ameitaka
Serikali kuweka suala la kodi katika mfumo unaoeleweka ili kumsaidia
mfanyabiashara kujua ni kiasi gani anatakiwa kulipa kwa mwezi.
Naye
Mbunge wa Temeke Abasi Mtevu amezitaja changamoto zinazowakabili
wafanyabiashara hao ni suala la usafi wanalipia lakini mazingira bado ni
machafu na wamesema wapo tayari kufanya usafi wenyewe na suala la zima
moto kwamba kila mfanyabiashara aweze kuwa na mtungi wa gesi lakini
hawapewi mitungi hiyo bali hupewa karatasi ya malipo.
Pia
amesema sheria zinazopitishwa Bungeni baadhi ni kweli na nyingine
zimetengenezwa na watu wenye maslahi binafsi na amewasisitiza
wafanyabiashara kupambana katika kulinda biashara pamoja na mitaji yao.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyabiashara wa Dar es Salaam (JWT), Philimon Chonde
akizungumza katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge
uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es
Salaam.
Mbunge wa Temeke, Mhe. Abas Mtemvu akisisistiza jambo katika mkutano wa
Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015
Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
Mbunge
wa Ubungo, Mhe. John Mnyika akifanya majumuisho katika mkutano wa
Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge uliofanyika leo Machi 5, 2015
Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wafanyabiashara akiombea mkutano kabla haujaanza.
Mbunge
wa Ubungo, Mhe. John Mnyika akisalimia na Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa
Azan Zungu katika mkutano wa Wafanyafanyabiashara pamoja na wabunge
uliofanyika leo Machi 5, 2015 Ukumbi wa Lamada Hoteli jijini Dar es
Salaam.
Waheshimiwa
wabunge wa jiji la Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini mkutano,
kutoka kulia ni Mhe. Abbas Mtemvu, Mhe. John Mnyika na Mhe, Mussa Azan
Zungu.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria katika mkutano huo.