SHABIKI WA WEMA SEPETU AWAJIA JUU MAADUI WAO AMBAO WALIOKUWA NA TABIA YA KUMTUKANA WEMA SEPETU

March 06, 2015


na hii ndo kauli ya shabiki huyo kupitia mtandao wa instagram anayetumia kina la @mrekebishatabia Naliongelea hili kwa mara ya mwisho...pls naomba msinifanye nisiwe huru kukoment popote au kuandika eti kwasababu unamchukia Wema Sepetu. Kuna watu nawaona kila nikiandika kitu au kuandika kwa wengine kama wametumwa lazima waandike eti uko team wema na mahubiri kibao!! Chuki zako kwa wengine ndo tushindwe kusapoti wengine? tafadhali!! Narudia kusema, nampenda Wema sio sababu ya teams na nini hapana ila kwasababu ni Wema kama

mtu mwingine yeyote, ni mwanadamu kama wewe, ana feelings kama nyie, maamuzi na mitazamo yake ni kama mwanadamu yeyote na kinachofanya nimpende zaidi ni kwasababu kuna groups za watu wanadhani watafanikiwa kumkosesha amani! Anatukanwa na wanayoyamtukana wengi wanayafanya hayo....kila mmoja wetu ana madhaifu yake huwezi kuwa busy unamtukana mtu yale yale ambayo unayafanya wewe tena na zaidi au kwa vile hatukuoni? Ila kwasababu ni Wema anabebeshwa mizigo na laana ya mambo unayofanya wewe!!! Seriously? Hapo kwanini asipendwe Wema anawakilisha wasichana wengi nchini. Mimi sikuzote nitasimama na yule ambaye watu wanamdharau na kumtukana bila sababu zozote za msingi. Lakini sio kila mada naandika its about them, pengine ni mifano ambayo iko wazi...sina upendeleo na kama naandika kitu kuna sababu.
CHANZO : 
makubwa haya blog

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »