Mwenyekiti wa kikundi cha Upendo
Family Group ,Faustine Mwanadago (kushoto)akimkabidhi msaada wa katoni
ya maji muuguzi mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru,Sifael
Masawe jana kikundi hicho kilipofanya ziara ya kutembelea wagonjwa
hospitalini hapo,jumla ya mashuka 300 na maji katoni 10 zenye thamani ya
zaidi ya sh,2 milioni zilikabidhiwa ,anayeshuhudia pembeni ni makamu
mwenyekiti wa kikundi hicho,Jasmine Kiure(Habari Picha na moses mashalla
wa jamiiblog.co.tz/)
Mwenyekiti wa kikundi cha Upendo
Family Group ,Faustine Mwanadago (kushoto)akimkabidhi msaada wa mashuka
na maji muuguzi mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru,Sifael
Masawe jana kikundi hicho kilipofanya ziara ya kutembelea wagonjwa
hospitalini hapo,jumla ya mashuka 300 na maji katoni 10 zenye thamani ya
zaidi ya sh,2 milioni zilikabidhiwa ,anayeshuhudia pembeni ni makamu
mwenyekiti wa kikundi hicho,Jasmine Kiure
Hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt Meru
inakabiliwa na upungufu mkubwa wa mashuka ya kujifunikia kwa ajili ya
wagonjwa mbalimbali waliolazwa hospitalini hapo hali ambayo imepelekea
baadhi ya wagonjwa hao kulala bila kujifunika nyakati za usiku.
Kwa sasa hospitali hiyo ina jumla ya vitanda 500 na mashuka 300 wakati wastani wa kitanda kimoja kinatakiwa kuwa na mashuka 8.
Akizungumza na waaandishi wa habari
mara baada ya kupokea msaada wa jumla ya mashuka 100 na katoni kumi za
maji kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa hospitalini hapo,muuguzi mfawidhi
wa hospitali hiyo,Sifael Masawe alisema kuwa tatizo la uhaba wa fedha
kutoka serikali kuu limechangia kukosekana kwa huduma mbalimbali
hospitalini hapo yakiwemo mashuka.
Alisema kuwa kwa nyakati tofauti
baadhi ya wagonjwa hushindwa kujifunika mashuka nyakati za usiku
kutokana na uhaba wa mashuka hayo na kuwataka wadau mbalimbali mkoani
Arusha kujitokeza kuokoa hali hiyo.
Akikabidhi misaada ya mashuka na maji
kwa ajili ya wagonjwa waliolazwa katika wodi wa akina mama hospitalini
hapo ,mwenyekiti wa kikundi cha Upendo Family,Faustine Mwandago alisema
kwamba misaada hiyo imegharimu kiasi cha zaidi ya sh,2 milioni.
Mwandago,alisema kuwa lengo la
kukabidhi misaada hiyo ni kuonyesha upendo kwa watu wenye mahitaji
mbalimbali sanjari na kulienzi jina la kikundi chao kwa vitendo huku
akiwataka wadau wengine kuwaunga mkono.
EmoticonEmoticon