Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akizungumzia migogoro ya
ardhi ya mkoa wa Morogoro ambapo kwa siku nzima ya leo alipata fursa ya
kusikiliza taarifa ya migogoro ya ardhi ya mkoa huo na kisha kupata
fursa ya kukusanya karatasi za kero za migogoro ya ardhi kisha
kuzikabidhi kwa timu ya wataalamu ambao watazichambua na kutoa
mapendekezo kwa waziri jinsi ya kuzitatua pia ameagiza ofisi za Msajili
wa Ardhi Kanda ya Mashariki kujengwa na kuhamishiwa Mororgoro.
Mbunge wa Viti Maalumu Susan
Kiwanga akizungumzia masuala ya migogoro yanayoukabili mkoa wa Morogoro
sambamba na njia ambazo zitasaidia kuondokana na migogoro hiyo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Morogoro, Amiri Nondo akifuatilia mjadala huo kulia kushoto kwake ni
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro, Innocent Kalogeris.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akizungumzia migogoro ya ardhi ya mkoa wa Morogoro
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akizungumzia migogoro ya ardhi ya mkoa wa Morogoro
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa
Morogoro, Leonard Paulo, akizungumzia changamoto zinazowakabili katika
kukabiliana na migogoro ya ardhi mkoani Morogoro.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, Lucy Nkya akizungumzia kero zinazowakabili katika eneo lao.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Morogoro, Innocent Kalogeris akizungumzia hali ya migogoro ya ardhi kwa
mkoa wa Morogoro wakati Waziri Lukuvi alipokuwa akisikiliza kero
mbalimbali za ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Morogoro.
Mbunge wa Ulanga Magharibi, Dk. Haji Mponda akizungumzia kero zinazowakabili katika eneo lao
a wa Morogoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Theresia Mahongo akikagua karatasi
zenye kero za migogoro ya ardhi zilizokuwa zikikabidhiwa kwake kwaajili
ya kukabidhi kwa Waziri Lukuvi.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akipokea makaratasi
yaliyoandikwa malalamiko ya wananchi wa mkoa wa Morogoro leo mchana
katika ziara yake aliyofanya mkoani humo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi William Vangimembe Lukuvi akipokea makaratasi ya
malalamiko ya wananchi wa mkoa wa Morogoro leo mchana katika ziara yake
aliyofanya mkoani humo kushoto kwake ni Mbunge wa Morogoro Mjini Aziz
Aboud.