RC BATILDA AWATAKA WAZAZI KUWA MAKINI NA WATOTO

March 22, 2026




Na Oscar Assenga, TANGA



MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi,Dkt Batilda Burian ametoa salamu za sikuu ya Eid El Fitri kwa wakazi wa mkoa huo huku akiwataka wazazi na walezi kuwa makini na watoto wanapotoka kwenda kutembea.



Dkt Batilda aliyasema hayo jana mara baada ya kumalizika kwa Swala ya Eid El Fitri iliyofanyika kwenye msikiti wa Ijumaa Jijini Tanga ambapo alisema ni muhimu wakati wa sikuuu wahakikishe watoto wanapokwenda kutembea wanakuwa na uangalizi.



Alisema kwamba kufanya hivyo kutawasadia kwenda kutembelea salama na kuweza kusheherekea sikuuu salama bila kadhia ambayo inaweza kuleta madhara mbalimbali ikiwemo majozi na msiba.



“Wazazi na walezi niwaombe Shehere ya Eid watoto wanakwenda kutembelea tuwe makini wawe na mtu mzima hata njiani wawe makini kuna vyombo vya usafiri bodabodoa na magari tuhakikishe tunakula sikuuu salama bila kadhia ambayo italeta msiba na majonzi”Alisema



Aidha aliwataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kudumisha amani na utulivu kuendeleza mshikamano kwa upendo pamoja na kuendelea kumuombea Rais wetu Dkt Samia Suluhu .



Mkuu huyo wa Mkoa alisisitiza wana Tanga kuendelea kuwaombea waliotangulia mbele za haki na waliojaliwa kuendelea kumshukuru Mwenyezi Mungu ikiwemo kuwaombea viongozi wa dini.



“Nitoe mkono wa Eid Fitri kwa wana Tanga na watanzania tuendelee kama tulivelekezwa tuwatembelee wagonjwa ndugu na jamaa na tuzuru makaburi na tufanye amali njema na tuendelee kupendana na kutenda mema”Alisema



Akizungumza Mbunge wa Jimbo la Tanga Kassim Amary Makubel aliwatakia heri ya sikuu ya Eid El Fitri wakazi wa Jiji hilo huku akieleza kwamba hivi sasa Tanga imefunguka kimaendeleo na itaendelea kufunguka zaidi kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali.



Mbunge huyo aliwashauri watu wa Tanga wasiwe wepesi wa kuunza nyumba zao hata kama ni za urithi na kama ikitokea anataka kuja Mwekezaji kuwekeza ingieni ubia kwa miaka fulani kwani watakapouza wanaweza kuwa nje ya mji.



Awali akizungumza Diwani wa Kata ya Ngamiani Kaskazini, Fahadi Rished amesema umoja ulioonyeshwa wakati wa swala ya Eid uendelee kushikamana na waendelee kuwasaidia ndugu na jamaa wasiojiweze.



Alisema kwamba kata yao ipo salama kwa wananchi kusheherekea sikuu ya Eid hivyo wananchi washeherekee kwa salama .


Mwisho.








Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »