SERIKALI KUIMARISHA MAZINGIRA WEZESHI YA UPATIKANAJI WA MAFUTA NCHINI- MHE KAPINGA

January 20, 2025

 


📌 *TBS kujenga Maabara ya kupima  ubora wa mafuta katika bandari ya Tanga.*


Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeahidi kuendelea kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha kuwa bidhaa za mafuta ya petroli, dizeli pamoja na mafuta ya taa nchini zinapatikana muda wote zikiwa katika ubora stahiki.



Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati wa uwasilishaji wa  taarifa ya hali ya uhifadhi wa mafuta nchini katika Bohari za Tanga na Mtwara kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Jijini Dodoma, Januari 20, 2025.



“Serikali ipo katika taratibu za kuboresha miundombinu ya upokeaji na uhifadhi wa bidhaa za mafuta katika Bandari za Tanga na Mtwara ili kuendana na ukuaji wa mahitaji ya bidhaa za mafuta katika maeneo hayo.” Amesema Kapinga



Amesema Serikali inaendelea kushirikisha wadau mbalimbali katika sekta ya mafuta ili kuhamasisha uwekezaji wa miundombinu ya upokea mafuta katika Bandari za Tanga na Mtwara ikiwemo kampuni binafsi zenye bohari za bidhaa za mafuta. 


Vile vile, Kapinga amesema kuwa Serikali kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) inaendelea  na ujenzi wa Maabara ya kupima ubora wa mafuta katika Bandari ya Tanga ili kufupisha muda wa kupata majibu ya vipimo vya ubora wa bidhaa hizo. 



Aidha, Serikali kupitia shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) inaendelea na mikakati ya uwekezaji wa Bohari ya bidhaa za mafuta katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mkoa wa Dodoma. 


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. David Mathayo David ameipongeza Wizara ya Nishati, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kwa kuendelea kuimarisha mazingira wezeshi ya upatikanaji wa bidhaa ya mafuta nchini.



Kwa kuendelea kuimarisha miumbombinu mbalimbali ya uzalishaji, usambazaji na usafirishaji wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini.



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »