Mwandishi Wetu, Kigamboni.
MWENYEKITI wa Mtaa wa Mbwamaji uliopo Gezaulole Kata ya Somangila Wilayani Kigamboni, Mhe. Yohana Luhemeja 'Maziku' ameanza kwa kishindo katika kuhakikisha anatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kupeleka maendeleo kwa Wananchi ameendesha zoezi la uchongaji wa barabara 8, zinazoingia na kutoka katika Mtaa huo.
Zoezi hilo lililoanza mapema jana Januari 19, 2025, uchongaji wa barabara hizo zenye urefu wa Kilometa mbili (KM2) kila moja ikiwemo pia kuweka sawa kwa kufukia madimbwi na vifusi ambayo yalikuwa kero.
"Zoezi hili la ukachongaji wa barabara linafuatia kikao changu cha kwanza nilipoapishwa tu, kuahidi kuanza na kero hii. Tumeanza rasmi Januari 19, na litafikia tamati kesho Januari 21,2025. Tumeanza na barabara hizi Nane kwanza, baadae tunaendelea na zingine.
Tunashukuru Halmashauri ya Manisapaa ya Kigamboni kupitia kwa Mkurugenzi kupitia kwa Diwani wetu wa Kata ya Somangila kwa kutupatia greda na sie Ofisi yetu imeweza kuratibu mafuta na nguvu kazi kwa kushirikiana na Katibu wa CCM tawi, Kamati ya Ardhi ya Mtaa na Kamati ya Miundombinu ambazo tumefanikisha kuhakikisha lengo la kusukuma maendeleo mbele.
Tumeanza barabara hizi nane, lakini pia zingine Nne tunaendelea nazo hapo baadae. Lengo kuhakikisha Mtaa wa Mbwamaji Wananchi wanaingia na kutoka bila kero ya Miundombinu.". Amesema Mhe. Maziku.
Aidha, Mhe.Maziku amebainisha kuwa, ataendelea kupambania Wananchi wa mtaa huo ikiwemo kuwasogezea Huduma muhimu za Maji, Afya, elimu na Soko.
"Tunaendelea kuwashukuru viongozi wetu wa juu wa Chama na Serikali kwa kupeleka maendeleo ngazi ya chini, Mbwamaji tunamhakikishia Mhe Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan anapata kura za kishindo katika uchaguzi hapo baadae mwaka huu,
Mbwamaji ya maendeleo ipo tayari tuungane kwapamoja". Amesema Mhe. Yohana Luhemeja 'Maziku'.
Mtaa huo wa Mbwamaji ni miongoni mwa mitaa mikongwe hapa nchini wenye historia ya kipekee ikiwemo kuwa na Kijiji cha kale, Mtaa ambao pia umezungukwa fukwe ya bahari ya Indi.
Mwisho.
EmoticonEmoticon