Muonekano wa uwanja wa Simba sc uliopo eneo la Bunju jijini Dar es salaam
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TANGU Simba sc ianzishwe miaka ya 1930’s haijawahi
kulimika uwanja wake wa mazoezi wala uwanja wa mazoezi ukilinganisha na Azam fc
iliyoanza kushiriki ligi kuu Tanzania
bara kwa mara ya kwanza msimu wa 2008/2009
Hii ni historia mbaya kwa klabu kubwa kama Simba
ambayo wakati wa kuanzishwa kwake ilikuwa inaitwa Queens, baadaye Eagles, Dar
Sunderland na mwaka 1971 ilibadilishwa jina na kuitwa Simba Sports Club.
Simba yenye historia kubwa ya soka la Tanzania sasa
ipo katika mchakato wa ujenzi wa uwanja wake, lakini leo katika hotuba yake,
Rais wa klabu hiyo, Evans Elieza Aveva amewahakikishiwa wanachama wa Simba kuwa
miezi michache ijayo, klabu itamiliki
uwanja wake wa mazoezi.
Uongozi wa Ismail Aden Rage ulianza utekelezaji wa
ujenzi wa uwanja wa mazoezi eneo ya Bunju jijini Dar es salaam na sasa
maendeleo ni mazuri ambapo nyasi zilizopandwa na zinaendelea kuota.
Aveva alisema uongozi wake umetengeza zaidi ya
shilingi milioni 600 ili kukamilisha ujenzi wa uwanja wa mazoezi.
Pia Simba ipo katika mpango wa kujenga Hosteli za wachezaji ili kuepukana na gharama kubwa wanazotumia kuwaweka wachezaji Hotelini.
EmoticonEmoticon