KATIKA kukabiliana na tatizo la maji katika kata ya Kwediboma iliyopo wilayani Kilindi serikali imetenga kiasi cha sh. Bilion 2.8 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji safi kwenye vijiji kumi vinavyounda kata hiyo.
Rais Kikwete amebainisha hayo jana wakati akihutubia wananchi wa kata ya Kwediboma kabla ya kuzindua ujenzi wa mradi wa Maji ya Bomba wa kijiji cha Kwediboma unatekelezwa kupitia mpango wa kuendeleza sekta ya maji kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania.
![]() |
"Ndugu zangu pamoja na serikali kuwekeza fedha hizi tambueni kwamba kama jamii mnalo jukumu kubwa la kuhakikisha mradi huu unatunzwa ili uwe endelevu kwa ajili ya kutoa huduma kwenu na vizazi vijavyo...naomba wananchi waote washiriki kutimiza jukumu hili ili kutoa huduma endelevu", alisema rais.
Vijiji vitakavyonufaika na huduma ya maji kupitia fedha hizo ni
Mpalahala, Kwedigole,Kileguru,Mzinga ambavyo kwa sasa havina huduma ya maji hasa baada ya ya chanzo chao tegemezi ambacho kilikuwa ni Malambo mawili yaliyojengwa na halmashauri kupitia mradi wa DADPS kubomolewa na mvua msimu uliopita. Ibrahim Abdallah alisema hadi kukamilika kwake unatarajiwa kugharimu kiasi cha sh. 517,364,391 na kwamba mpaka sasa zimetumika sh. 316,197,327 kwa ajili ya kukamilisha kazi za awamu ya kwanza ya mradi.
""Mradi huu unaotarajiwa kunufaisha wakazi 7,139 wa kijiji cha
Kwediboma ulianza mwaka 2010 baada ya kuibuliwa na wananchi ....katika awamu ya pili iliyoanza mwaka 2013 tulijenga miundombinu pamoja na vituo 24 vya kusambazia maji kijijini, nyumba ya kuhifadhia mitambo ya kusukumia maji toka kwenye chanzo , tangi, kufunga dira", alisema.
Katibu huyo alisema kubomoka kwa malambo hayo tayari kulisababisha ugomvi mkubwa baina ya wakulima na wafugaji ambao wamekuwa wakihama hama kusaka malisho.
EmoticonEmoticon