RAIS Jakaya Kikwete amewaonya watendaji wa vijiji na kata kuacha kupokea rushwa ya Mbuzi na Kondoo ili kuwaruhusu wafugaji kuingia kwenye maeneo yao kwani kufanya hivyo kunapelekea kuibuka migogoro kati ya wakulima na wafugaji hali inayotishia usalama wa wananchi hao.
Kauli hiyo ya Mkuu wan chi alitoa wakati akiwahutubia wananchi wa wilaya ya Pangani kwenye uwanja wa Sakura akiwa katika ziara yake wilayani hapa iliyoambatana na uzinduzi wa miradi ya maendele.
Alisema kimsingi suala la migogoro hiyo inachagiwa na viongozi hao ambao wamekuwa wakishindwa kuweka mipango imara ambayo inaweza kuyapatia ufumbuzi matatizo hayo kwa kugeuka kuwa chanzo chake hali inayopelekea wananchi kuichukua serikali.
“Mimi naambieni watendaji wa vijiji na kata ambao mnachangia
kuwepo migogoro kwenye maeneo yenu acheni tabia hiyo mara moja kwani ukibainika hatutaweza kukuvumilia lazima uchukuliwe hatua zinazostahili kumaliza tatizo hilo “Alisema Rais Kikwete.
Aidha alisema kuwa sio kama viongozi hao wanashindwa kuweka mipango mizuri ya kulipatia ufumbuzi tatizo la migogoro ya ardhi bali miongoni mwao wamekuwa wakichangia hali hiyo kwa kuwakaribisha wageni kwenye maeneo yao bila kufuata taratibu zilizopo.
Akizungumzia suala la mifugo kwenye maeneo ambayo yameonekana kuwa na misuguano ya mara kwa mara Rais Kikwete alisema umefika wakati wa viongozi wake kuyatafutia ufumbuzi kwa kuweka utaratibu utakaowezesha kuondoa kero hizo.
Aliongeza kuwa katika jambo hilo Serikali imeweka mpango mkakati kwa mkoa mzima wa Tanga ambao utasaidia kupunguza tatizo la ardhi ili kuwapa fursa wananchi kufanya shughuli za kimaendeleo badala ya kuendelea kufikiria namna ya kutatua tatizo hilo.
Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa mikoa hapa nchini inayokabiliwa na migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji ambao hupelekea wakati mwengine kupelekea mapigano ikiwemo kuharibu miundombinu iliyopo kutokaa na ufinyu wa ardhi.
Aliwataka viongozi kutengeneza utaratibu mzuri ambao hautaleta
migogoro kwenye maeneo ambayo wafugaji hao wanaoishi ili waweze kuishi kwa utulivu ikiwemo kuzitaka kamati za ulinzi na usalama za wilaya ya mikoa kuhakikisha wanazipatia ufumbuzi kero hizo.
EmoticonEmoticon