CLABU ya Ako Labamba ya jijini Dar es Salaam imejitosa
kudhamini shindano la Miss Ubungo litakalofanyika mwezi ujao.
Baadhi ya washiriki wa Miss Ubungo 2014 wakiwa katika pozi.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja Miradi wa
Kampuni ya AKO Group Ltd, Honesty Minde, alisema wameamua kudhami ni shindano
hilo ili kusaidia kulifanikisha.
Alisema wameamua kuwasaidia waandaaji wa shindano hilo ili
kukuza sanaa ya urembo, wakiamini kuwa ndio dira ya maendeleo kwa Watanzania
wote.
Baadhi ya washiriki wakiwa katika pozi kwenye clabu ya Ako Labamba.
“Tuliamua kuwapa maeneo ya kufanya mazoezi pamoja na huduma
nyingine muhimu kwa waandaaji na warembo wao. “Naamini kwa pamoja tutafanikisha kwa vitendo mafanikio
makubwa ya Miss Ubungo mwaka huu, ukizingatia kuwa ndio lengo letu,” alisema.
Wadhamini wengine katika shindano hilo ni Sigmark Tanzania, Prima
Hair, Smart Bol, Handeni Kwetu Blog, MG Hostel, City Park Hotel, Milladayo.com,
Dartalk na Nelson Fashion.
EmoticonEmoticon