DKT.NCHIMBI -DKT SAMIA AMEPAISHA BAJETI SEKTA YA UVUVI,APEWE MITANO TENA

October 20, 2025


Mgombea mwenza wa Kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uongozi wake ndani ya miaka minne ameleta mageuzi makubwa katika Sekta ya Uvuvi kwa kuiongezea bajeti zaidi ya mara sita ili iweze kuwa na tija.

Dkt Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Oktoba 20, 2025 wakati akiwahutubia  Wananchi kwenye mkutano wake wa kampeni za Urais katika jimbo la Kilwa Kaskazini, Mkoani Lindi, ambapo amenadi  Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2025-30, Sera zake pamoja na kumuombea Kura Dkt Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani kwenye kanda hiyo ya kusini.

"Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Uvuvi hasa kwa mkoa wa Lindi ni pamoja na kujengwa kwa Bandari ya Uvuvi iliyogharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200" amesema Dkt Nchimbi.

Katika hatua nyingine Dkt.Nchimbi alitumia nafasi hiyo pia kuwanadi wagombea Ubunge wa mkoa huo,akiwemo mgombea Ubunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini Ndugu Kinjeketile Ngombale MWIRU na mgombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kusini Ndugu Hasnain Gulamabbas DEWJI pamoja na Madiwani





Share this

Related Posts

Previous
Next Post »