SOKO LA MICHUNGWANI LITAPUNGUZA UMBALI KWA WAKAZI WASIOPUNGUA 13,513 MUHEZA

April 08, 2014
NA OSCAR ASSENGA,MUHEZA.
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Ibrahimu Matovu amesema ujenzi wa soko la michungwani wilayani hapo litasaidia kupunguza umbali kwa wakazi wasiopungua 13,513 wa maeneo ya kata za Genge na Majengo ambao awali walikuwa kupata mahitaji yao katika soko kuu la Muheza mjini.


Matovu aliyasema hayo jana wakati akizungumza na TANGA RAHA BLOG ambapo alisema mradi huo utatoa fuksa kwa wafanyabiashara wadogo 48 kupata meza za kuuzia bidhaa za awamu ya pili itakapokamilika pamoja na kuongeza mapato ya mtu mmoja mmoja na halmashauri kutokana na ushuru. Soko hilo lina majengo makubwa matatu ikiwemo la mbogambogo na matunda,nafaka na wauzaji wa jumla ,vibanda vya ofisi,maduka na migahawa ya kuzunguka soka zima kwa wafanyabishara watakaokwenda kuuzia bidhaa zao hapo. Alisema soko hilo limegharimu kiasi cha sh.milioni 224,808,754 ambapo jengo la kwanza limejengwa kwa awamu pili na wakandarasi tofauti ambao ulianza mwaka 2011 na kumalizika mwishoni mwa mwaka huo. Awamu ya kwanza ya ujenzi wa jingo kuu hadi kupaua chini ya mkandarasi aitwae Masai Construction&General Supply Ltd kwa mkataba Na.MUH/DC/LGCDG/10/11/02 wakati awamu ya pli ilihusisha umaliziaji wa soko na ujenzi ulikamilika mwaka jana kupitia mkandarasi Fair Class Construction Ltd wa Morogoro kwa mkataba wa Na.MUH/DC/LGCDG/2011/2012/05 wenye thamani y ash.milioni 112,607,154. Aliongeza kuwa mradi wa soko la mboga mboga na matunda limegharimu kiasi cha sh.milioni 102,381,600 kwa mkataba wa namba LGA/MDC/CTB/LGCDG/2012/2012/10 chini ya mkandarasi Cooperation Sole Works.
Hata hivyo mkurugenzi huyo alisema halmashauri hiyo katika mipango yake ya baadae wana mipango ya kujenga jingo la kuchambua ,kufungashia na kuhifadhi matunda ambao mradi huo unatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa kutumia fedha za DADPS.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »