BARRICK BULYANHULU SPORTS CLUB YATWAA UBINGWA WA BONANZA LA MEI MOSI SHINYANGA

May 03, 2026
Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Barrick Bulyanhulu Sports Club akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa Bonanza la Mei Mosi.
Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Barrick Bulyanhulu Sports Club akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa Bonanza la Mei Mosi.
Nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Barrick Bulyanhulu Sports Club akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, baada ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa Bonanza la Mei Mosi.
Mchezo wa fainali ukiendelea kati ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Mgodi wa Dhahabu Barrick Bulyanhulu Sports Club na Kahama Manispaa (MC), ambapo Barrick Bulyanhulu iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kutwaa ubingwa wa mashindano ya Wiki ya Mei Mosi yaliyofanyika Uwanja wa Taifa Kahama.
Mchezo wa fainali ukiendelea kati ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Mgodi wa Dhahabu Barrick Bulyanhulu Sports Club na Kahama Manispaa (MC), ambapo Barrick Bulyanhulu iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kutwaa ubingwa wa mashindano ya Wiki ya Mei Mosi.
Timu ya mpira wa miguu ya Mgodi wa Dhahabu Barrick Bulyanhulu Sports Club imetwaa ubingwa wa mashindano ya Wiki ya Mei Mosi baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kahama Manispaa (MC) katika mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Taifa Kahama.

Akizungumzia ushindi huo, Nahodha wa timu hiyo Juma Mbamba alisema mafanikio hayo yametokana na nidhamu, kujituma pamoja na kufanya mazoezi ya mara kwa mara.

“Barrick tunathamini michezo kwani tunaamini ina mchango mkubwa katika kujenga afya za watumishi wetu. Ndiyo maana viongozi wetu wameweka mikakati ya kuhakikisha watumishi wanafanya mazoezi mara kwa mara na kushiriki katika michezo mbalimbali,” alisema Mbamba.

Baada ya ushindi huo, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita, aliipongeza timu hiyo na kutoa zawadi ya fedha taslimu kiasi cha shilingi milioni moja kama hamasa kwa ushindi walioupata.

Mbali na zawadi hiyo ya fedha, timu hiyo pia ilikabidhiwa kikombe cha ubingwa, seti ya jezi pamoja na mipira miwili ikiwa ni sehemu ya kutambua juhudi zao.

Wakati huohuo, timu ya mpira wa pete kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga (RAS Sports Club) iliibuka mabingwa baada ya kuifunga timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama katika mchezo wa fainali.

Bonanza hilo liliandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani maarufu kama Mei Mosi, ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 1 Mei.



Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »