NAIBU WAZIRI JANETH MBENE AFUNGUA MAFUNZO YA WADADISI WA ZOEZI LA SENSA YA VIWANDA
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bw. Eliya Ntandu akizungumza kwa niaba ya
Makatibu Tawala wa mikoa yote nchini wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya
Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda uliyofanyika leo
mkoani Morogoro.
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akitoa maelezo
mafupi kuhusu Sensa ya Viwanda wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi
na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda uliyofanyika leo mkoani
Morogoro.
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene akiwa katika mahojiano
maalum na waandishi wa habari baada ya kufungua rasmi mafunzo ya
Wadadisi na Wasimamizi wa Zoezi la Sensa ya Viwanda yaliyofanyika leo
mkoani Morogoro.
Baadhi
ya wadadisi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi (hayupo
pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Wadadisi na Wasimamizi wa
Zoezi la Sensa ya Viwanda uliyofanyika leo mkoani Morogoro.
……………………………………………………………………………………..
Na Veronica Kazimoto, Morogoro
Wamiliki
wa viwanda nchini wameagizwa kutoa taarifa sahihi na ushirikiano wa
kutosha wakati wadadisi watakapofika katika ofisi zao kuwahoji kwa ajili
ya kupata takwimu za viwanda vyao.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya wadadisi na wasimamisi wa zoezi la
Sensa ya Viwanda iliyofanyika leo mkoani Mororgoro, Naibu Waziri wa
Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene (Mb) amesema ni muhimu wamiliki wa
viwanda kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wadadisi kwa kuwa takwimu
zitakazopatikana kutokana na Sensa hiyo zitatumika katika kupanga
shughuli mbalimbali za maendeleo.
“Nichukue
Fursa hii kuwaagiza wenye viwanda wote nchini kuona kuwa zoezi hili ni
lao na ni jukumu lao kutoa taarifa sahihi kwa wadadisi na pia waone kuwa
zoezi hili ni kwa ajili ya manufaa yao na taifa kwa ujumla.” Amesema
Naibu Waziri Mbene.
Naibu
Waziri Mbene amefafanua kuwa, zoezi hili la Sensa ya Viwanda
lisichukuliwe kama njia ya Serikali kutaka kujua mapato au faida
wanayopata wenye viwanda kwa lengo la kukusanya kodi bali ni kuisaidia
Serikali kubaini mabadiliko ya muundo wa sekta ya viwanda, mchango wake
kwenye pato la taifa na hatimaye kufanya maamuzi sahihi ya kisera.
Aidha
ametoa wito kwa wadadisi wote wanaoshiriki katika mafunzo ya Sensa ya
Viwanda kufuatilia na kuzingatia kwa makini mafunzo yote yatakayotolewa
na wakufunzi ili lengo la kupata takwimu sahihi za viwanda liweze
kufanikiwa.
Awali
akitoa maelezo ya utangulizi Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema takwimu zitakazokusanywa katika Sensa
hiyo zitahusu viwanda vidogo, vya kati na vikubwa.
Dkt.
Chuwa amefafanua kuwa katika sensa hiyo baadhi ya taarifa
zitakazokusanywa ni pamoja na anuani na mahali viwanda vilipo, aina ya
umiliki, utaifa wa mmiliki, mwaka kiwanda kilipoanzishwa, aina ya bidhaa
zinazozalishwa na idadi ya wafanyakazi.
Taarifa
nyingine ni gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mapato
yanayotokana na uzalishaji, gharama za uzalishaji na mapato mangineyo.
Mafunzo
ya zoezi la Sensa ya Viwanda yamelenga vijana wapatao 175 ambao
watafanya kazi ya kukusanya takwimu zinazohusu sekta ya viwanda hapa
nchini kwa muda wa miezi miwili kuanzia mwezi Aprili mpaka Juni 2014.
EmoticonEmoticon