KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS, SAAZ SALULA, AKAGUA MIRADI YA HIFADHI YA ZIWA TANGANYIKA MKOANI RUKWA
Safari
ya msafara wa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Salula
mwishoni mwa juma katika kukagua miradi inayofadhiliwa na Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira pamoja na wahisani wengine katika Wilaya ya
Kalambo Mkoani Rukwa haikuwa rahisi kutokana na kukabiliwa na changamoto
ya barabara kutokana na mvua kubwa kunyesha na hivyo kupelekea magari
ya mizigo inayokwenda nchi jirani za Burundi na DRC kupitia bandari ya
kasanga kukwama na kuziba njia. Juhudi za ziada kwa kushirikiana na
wananchi pamoja na mkandarasi anaejenga barabara hiyo ya Sumbawanga –
Kasanga kwa kiwango cha lami zilisaidia katika kuhakikisha magari yote
yaliyokwama pamoja na msafara wa katibu Mkuu yanavuka salama.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Salula (watatu kulia) akiwa na msafara wake wakielekea kagua wadi ya kujifungulia kinamama kijiji cha Samazi Wilayani Kalambo ikiwa ni sehemu ya mradi unaosimamiwa
na mradi wa hifadhi wa ziwa Tanganyika uliopo chini ya Ofisi ya Makamu
wa Rais Mazingira pamoja na miradi mingine ya ujenzi wa vyumba vitatu
vya madarasa katika shule ya msingi Muzi na ujenzi
unaoelekea kukamilika wa daharia (bweni) katika shule ya sekondari
Kasanga. Katika msafara wake aliambatana na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa
Ndugu Smythies Pangisa (wa nne kulia)
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Salula akizungumza na mhudumu
wa afya katika wadi ya wazazi Samazi juu ya huduma na mahitaji ya kituo
hicho kipya ambacho kinategemewa kuanza kazi siku za hivi karibuni.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na msafara wake wakikagua vitanda kwa
ajili ya wanafunzi pamoja na daharia katika shule ya Sekondari Kasanga
Mkoani Rukwa. Mradi huo wa daharia (bweni) ni kwa ajili ya wanafunzi wa
kike katika Shule hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimkaribisha Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Salula katika Wilaya yake kwa
ajili ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa soko la samaki la
Kirando linalofadhiliwa na mradi wa usimamizi wa Ziwa Tanganyika uliopo
chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuonyesha Katibu Mkuu Ofisi
ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Salula (wa pili kushoto) sehemu inapojengwa
gati kwa ajili ya kushushia samaki na abiria katika soko hilo pamoja na
eneo linalojengwa kwa ajili ya kukaushia samaki wabichi. Kulia ni
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa.
Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akimuongoza Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais na msafara wake katika kukagua ujenzi wa miundombinu
inayoendelea kujengwa katika soko la samaki la Kirando Wilayani Nkasi
Mkaoni Rukwa mwishoni mwa juma.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Ndugu Saaz Salula akitoa baadhi ya
maelekezo kwa mkandarasi wa Soko la Samaki la Kirando ambae pia anajenga
Gati linaloonekana kwa ajili ya kuunganisha huduma katika soko hilo na
bidhaa za samaki zinazotoka ziwani (Ziwa Tanganyika).
Gati linaloendelea kujengwa kwa ajili yakuhudumia soko hilo la samaki la Kirando wilayani Nkasi.
(Na Hamza Temba – Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @ rukwareview.blogspot.com)
EmoticonEmoticon