MAKANGE SIUNGI MKONO SERIKALI TATU.

February 02, 2014
Na Oscar Assenga, Tanga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Mrisho Kikwete ni kiongozi ambaye  anapaswa kupongezwa kwa dhamira yake ya thati ya kuhakikisha anawapatia watanzania Katiba Mpya hii inaonyesha kwamba ni msikuvu mwanademokrasia makini na mtu asiyeogopa mabadiliko.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga(UVCCM)Abdi Makange wakati akizungumza na mwandishi wa makala hii ambapo anasema Rais Kikwete  katika suala hilo angeweze kuacha kuwapatia watanzania katiba mpya lakini akaona bora afanye hivyo.

Makange anasema wao kama umoja wa wa vijana wanampongeza sana pamoja na kumpongeza kwa mazuri yaliyomo kwenye katiba mpya ambapo anasema binafsi haungi mkono suala la serikali tatu kwa sababu haoni kama inatija kwa watanzania hapa nchini.

Anasema suala la Katibu mpya linahitaji umakini mkubwa sana ingawa hakupata bahati ya kuisoma kiundani zaidi kwa kusema ina mazuri yake na mambo yasiyokuwa mazuri likiwemo suala la serikali tatu ambalo litaweza kurudisha nyuma maendeleo nchi.


Anafafanaua kuwa serikali tatu ina maana kuwa asilimia kubwa ya watu waliokataa serikali tatu ambao hawajaonyesha kwenye ripoti zilizopo.

Makange anasema yenye binafasi suala la katiba mpya analiunga mkono kwa asilimia kubwa lakini msimamo wake upo kwenye tamko ambalo walilitoa wao kama UVCCM mkoa wa Tanga la kutaka serikali mbili na sio tatu kama linavyoelezwa na wanasiasa mbalimbali hapa nchini.

Anaeleza kuwa sababu za kukataa serikali tatu,Makange anasema sababu kubwa ni inatupeleka kwenye mgawanyiko wa undugu wetu na urafiki wetu lakini pia ni kuvunja misingi iliyowekwa na mwasisi wa Taifa hili hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere ambayo ni tunu kwa nchi yetu.

Mwenyekiti huyo anasema kitendo  kinaonyesha kinataka kuzoofisha juhudi za mwalimu Nyerere kwa maana kuwa tunapokwenda kwenye serikali tatu tunaodhofisha muungano pamoja na kutoa mwanya kwa wadau wa ndani kuweza kuuvunja muungano siku akitokea Rais mwendawazimu kwa upande
mmoja na kuuvunja muungano.

Anasema kuwa hawaungi mkono juhudi zozote za kupelekea kuuvunja muungano kwa sababu serikali tatu ni kuuvunja muungano likiwemo ukubwa wa gharama za uendeshaji inawezekana zikatoka upande mmoja hivyo kupelekea hasara kwa kutumia sana rasilimali za serikali ile kujiendesha.

Naamini watanzania  wa leo wanataka katiba mpya ambayo itaelezea vizuri namna ya kufaidika na rasilimali za nchi hii ikiwemo suala la gesi,madini  na wanyamapori na mengine mengi kupitia katiba mpya watanzania watafaidika.

Makange anasema watanzaia pia wanataka kujua mamna gani
watawashughulikia mafisadi,wahujumu uchumi lakini mimi siamini kwa kuwa sarakasi zisizo na msingi kwa kuibomoa dola ni kuunda serikali tatu ambayo inaonekana dhahiri inatupeleka watanzani mahala ambapo sio pazuri.

Akizungumzia hali ya kisiasa hapa nchini,Makange anasema Chama cha Mapinduzi (CCM) bado kina nguvu kubwa kwenye nchi hii kutokana na mipango yake na sera walizojiwekea kuwahudumua watanzania wapatao milioni 45 kwenye nchi hi kuhakikisha wanapata elimu nzuri na huduma za afya.

Anaeleza ukiangalia kwa asilimia kubwa utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi unatekelezwa kwa asilimia kubwa sana akitolea mfano kwa mkoa wa Tanga ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010.

Suala la uchumi ukiangalia ilani ya uchaguzi ibara ya 19 lengo la
ibara hiyo ilikuwa ni kujenga msingi wa uchumi wa kisasa kwa Taifa linalotegemea kwa kujenga pamoja na kukua kwa uchumi wa nchi  ambapo kwa mkoa wa Tanga umeandaa mpango wa utekelezaji mpango wa uwiano wa miaka 5 kuanzia mwaka 2011 mpaka 2016.

Katika kukuza uchumi anasema maana yake anazungumzia kukua kwa mapato ya mtu mmoja mmoja na kuendeleza huduma za kijamii ikiwemo sekta ya elimu kwa kuongeza ufaulu  ,tatizo la maji kuhakikisha maji yanapatikana kwa ukaribu na kuendelea kuboresha huduma za afya na tiba (CHF) mpaka kufikia asilimia 50 2015.

Aidha hakusita kulizungumzia pato la mkoa wa Tanga anasema kwa mujibu wa takwimu za ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS)  2011  pato ghafi la mkoa lilikuwa ni Trilioni 1.78 ambapo mpaka kufikia 2012 pato hilo limeongezeka na kufikia trilioni 2.009 hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 17.8%.

Anasema pamoja na kwamba wananchi hawataka kupata takwimu kwa makaratasi wanataka kuona kwa vitendo hali sasa wanaweza kumudu gharama za zao za maisha hilo ndilo ambalo linalowapelekea watanzania kuwa na imani na chama chao cha  Mapinduzi .

Hata hivyo anasema vyama vya kisiasa vya upinzani vipo na zinanguvu kwa baadhi ya maeneo na huwezi kukilinganisha na chama cha mapinduzi na hilo lipo kwa sababu hawafanyi kazi zao ipasavyo kwa wananchi wanaowaongoza .

Wakati tukiwa tunaendelea na maongezi yetu nilibahatika kumuuliza historia yake ya kisiasa ambapo Makange  anasema aliingia rasmi kwenye ulingo huo mwaka 2005 wakati akiwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Mkoani Morogoro kabla ya hapo alibahatika kusoma kwenye shule za wazazi zinazomilikiwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mombo ambapo wakati akiwa shuleni hapo alikuwa akipata nafasi ya kuingia kwenye siasa.

  “Nilivutiwa sana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwalimu Nyerere kwani  Rais Kikwete ana ndugu yake toka Mkoa wa Pwani,Sadiki Mwera ambaye alikuwa diwani Rufiji kwa sababu yenye alikuwa na hamasa kubwa ya siasa  na alipokuwa anakaa naye akajikuta anahamasika kujiingiza kwenye siasa “Anasema Makange.

Anaelezea baada ya kupata hamasa hiyo ya kisiasa  wakaona waanzishe matawi ya Chama cha Mapinduzi  ndani ya Chuo cha Mzumbe wakishirikiana na Anthony Mavunde ambaye sasa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu mkoani Dodoma(MNEC) ,Fredick Mushi  ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana chama cha Mapinduzi (UVCCM)Mkoa waKilimanjaro,Mohamed Nyundu na MNEC wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa huo pamoja na Ado Novemba ambao walikuwa chachu ya uanzishwaji wa tawi hilo.

Makange anasema baada ya kumaliza Chuo mwaka 2008 alirudi wilayani Korogwe ambapo alikutana na Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) ukiendelea akaamua kuomba nafasi ya Mjumbe wa Mkutano wa Mkoa ambapo alifanikiwa kupata nafasi hiyo ya mjumbe mpaka 2012.

Anasema mwaka 2012 ulipojitokeza uchaguzi mwengine ya umoja huo akaona akijitokeza kuwania nafasi ya Uenyekiti wa Mkoa wa Tanga ndipo alipofanikiwa kuipata na kuishikilia mpaka wakati huu akiwa na matazamio ya kutaka kutoka kwenye nafasi hiyo na kwenda kuwatumikia wananchi.

Akizungumzia suala la Urais ,Makange anasema muda wa kulizungumzia hilo bado haujafika kwa sababu bado nchi yetu  ina rais aliyepo madarakani kwa sasa hivyo tumuache amalize kazi zake na kuwataka wasubiri mwezi mei 2015 ndio ambapo mgombea urais atajulikana .

Halikadhalika Mwenyekiti huyo ambaye pia ni Katibu wa Afya wa
Halmashauri ya Jiji la Tanga,anasema wakati huu sio wa makundi bali ni kushikamana pamoja ili kukijenga chama hicho pamoja na kufanya kazi za kumsaidia Rais Jakaya Mrisho Kikwete ili kuweza kutekeleza ilani  ya Chama.

Anasisitiza kuwa yenye kama Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Tanga ni kuhakikisha chama hicho kinashinda kwenye chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka 2015 ili kuweza kupata ridhaa ya kuwatumikia wananchi wao.

Makange ambaye ni mzaliwa wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga anasema kuwa malengo yake makubwa ni siku moja kupata ridhaa ya kuwatumia wananchi wa wilaya hiyo na anaamini kuwa wana korogwe wanamaamuzi yao kwani ukienda wilayani humo ukiwauliza vijana changamoto kubwa waliokuwa nazo ni ukweli usiopingika wanahitaji mtu wa kuwatatulia changamoto zao.

Hata hivyo anaeleza kuwa malengo yake ni kuwa siku moja kupata ridhaa ya kuwatumikia wananchi wa wilaya hiyo hasa kwenye chombo cha kutunga sheria kama ilivyo matumini ya chama chochote cha siasa kushika dola .

Mwisho
Mwandishi wa Makala hii anaitwa Oscar Assenga wa Tanga.
Anapatikana kupitia  +2550714543839/0754000186 emailiadress
assengaoscar@gmail.com ua website www.assengaoscar.blogspot.com

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »