DC DENDEGO NA DIWANI SELEBOSI WAPANIA KUINUA VIPAJI VYA WANAMICHEZO WILAYANI TANGA.

February 02, 2014



Picha hizo ni Kikundi cha Majuto Arts Group wakionyesha umahiri wao
kwenye bonanza la Michezo ambalo limeandaliwa na Mkuu wa wilaya ya
Tanga Halima Dendego kwa kushirikiana na Diwani wa Kata ya Nguvumali
Mustapha Selebosi ambapo bonanza hilo hufanyika kila Jumamosi kwenye
viwanja vya shule ya msingi Majani Mapana jijini Tanga.
Na Oscar Assenga, Tanga.
DHAMIRA ya Mkuu wa wilaya ya Tanga,Halima Dendego na Diwani wa Kata ya Nguvumali Mustapha Sellebosi ya kuinua vipaji vya soka kwa vijana inapaswa kuungwa mkono na wadau wengine mkoani Tanga kwani itasaidia kupunguza vitendo viovu na kuwaepusha kukaa vijweni.

Viongozi hao wawili waliamua kukaa na kuamua kuanzisha bonanza la michezo ambalo limekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wa wilaya ya Tanga ambalo hufanyika kila Jumamosi kwa kuwakutanisha wasanii chipukizi na timu mbalimbali za mpira wa miguu,pete,wavu na michezo mengine ikiwemo kukimbia na kuvuta kamba.



Bonanza hilo lilianzishwa rasmi mwishoni mwa mwaka jana linalofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi majani mapana ambapo huanza majira ya saa moja asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni kwa vijana kuonyesha vipaji vyao kupitia michezo mbalimbali.

Lengo lake liliwa kuwakusanya vijana pamoja ili kuweza kuwapatia elimu ya ujasiriamali vijana waliopo jijini Tanga ambalo pia hushirikisha wasanii chipukizi wa mziki bongofleva  kutoka wilaya za Tanga na Muheza.

Akizungumza na TANGA RAHA BLOG  kwenye bonanza hilo,Selle Boss anasema kupitia bonanza hilo wasanii wachanga kwenye tasnia ya mziki wa kizazi kipya hapa nchini wanapata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao na kuweza kuzionyesha kazi zao walizozifanya.

Anasema kupitia kamati ya bonanza hilo wanapata nafasi ya kuwalika wasanii wakubwa kwenye tasnia hiyo ambapo kwa mara ya kwanza walimualika msanii wa vichekesho Kingwendu ambaye alipata wasaha wa kutumbuiza

Hata hiyo,diwani huyo anasema wasanii wengine ambao walikwisha kupata nafasi ya kutumbuiza kwenye bonanza hilo ni Makamua kutoka Wakali Kwanza pamoja na wasanii chipukizi kutoka mkoani Tanga Hassani Husein "Mwandei",David Hassani "Mkongwe Rua",Dominick  Mndeme "D.Doctor,Fadhili Issa "Kidani" na Daudi Mabenya "Dady Beda"

Burudani nyengine hutolewa na wasanii Dulla wa Michano,Tunu
aliyetunukiwa ikiwemo maonyesho kutoka kwa vikundi mbalimbali vikiwemo vya sarakasi,kikundi cha mzee majuto na maigizo ambavyo hupata nafasi ya kuonyesha umahiri wao kwenye bonanza hilo.

Diwani huyo anasema washindi kwa kila mchezo wanapata nafasi ya kupatiwa zawadi mbalimbali ikiwemo Jezi,Medali na Mipira ambapo kwa mwaka jana washindi walikuwa wakipatiwa sabuni,vitenge na mafuta ya kupikia.

  "Bonanza hili limeweza kutoa ajira kwa vijana wapatao 45,000 kwenye kata yangu nah ii itaweza kuwakwamua vijana kimaendeleo pamoja na kuwaondoa vijiweni ambapo wanapokaa mara nyingi hufikiria kufanya vitendo viovu kwenye jamii zao "Anasema Sellebosi.

Aidha anazitaja timu ambazo zinashiriki kwenye bonanza hilo kwa upande wa mpira wa miguu kuwa ni Jogoo FC ya Mwambani, Kagera Shooting ya Nguvumali, Vasco Dagama ya Nguvumali, Masiwani Shooting ya Majengo, Sobber House Fc  ya Duga ,Chumbageni ,Veteran FC,Bandari FC.

Kwa upande wa mchezo wa Pete,Timu ya Halmashauri ya Jiji la Tanga,Timu ya Bonanza na Nguvumali ambapo ushindi kwenye mchezo huo umeonekana kuwa mkubwa sana kwa washiriki kucheza kwa jihadi kubwa ya kutaka kuzipa ushindi timu zao.

Katika mchezo wa wavu zipo timu za shule ya sekondari Galanosi,Chuo cha Euckenforde ,ABC,na Chuo cha Utumishi wa Umma cha Kange ambapo baada ya kumalizika michezo hiyo timu hiyo hupata nafasi ya kushiriki mashindano ya kuvuta kamba na kukimbia kwenye magunia.

Maonyesho mengine ambayo yamekuwa na kivutio kikubwa kwenye bonanza hilo ni vijana kucheza na pikipiki kwa staili ya aina yake kitendo ambacho kimepelekea hamasa ya mahudhurio ya vijana wa wilaya ya Tanga kuongezeka kila siku.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »