Wasafirishaji wahimizwa kutii sheria bila shuruti
Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akifungua rasmi ofisi ya SUMATRA
mkoa wa Singida.Kulia ni mstahiki meya wa manispaa ya Singida,Sheikh
Salum Mahami na katikati ni kaimu mkurugenzi wa SUMATRA Ahmed
Kilima.Picha na Nathaniel Limu.
Mkuu
wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone,akizungumza kwenye hafla ya
ufunguzi wa ofisi ya SUMATRA ya mkoa wa Singida.Kulia ni Kaimu
mkurugenzi mkuu wa SUMATRA Ahmed Kilima na kushoto ni meya mstahiki meya
wa manispaa ya Singida,Sheikh Salum Mahami.
Baadhi
ya wadau wa usafirishaji mkoa wa Singida,waliohudhuria hafla ya
ufunguzi wa ofisi ya SUMATRA mkoa wa Singida iliyofanyika mjini Singida.
Na Nathaniel Limu, Singida
MKUU
wa Mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone, amewahimiza wasafirishaji wa
abiria na mizigo kujenga utamaduni wa kutii sheria na kanuni bila
shuruti ili kujiepusha na faini mbali mali zinazopunguza mapato yao.
Dk.
Kone ametoa wito huo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye ufunguzi
wa ofisi ya SUMATRA mkoa wa Singida zilizoko kwenye majengo ya idara ya
ujenzi mjini hapa.
Amesema baadhi ya wasafirishaji wamekuwa wakilalamikia faini na adhabu za SUMATRA kuwa ni kali sana.
“Ningependa
kuwasisitiza wasafirishaji kuwa ili kuepuka faini, na adhabu kali
zilizowekwa na SUMATRA, inabidi kufuata sheria na kanuni zilizopo na si
vinginevyo” amesema na kuongeza;
“Nisingewashauri SUMATRA kupunguza adhabu ili kuwafurahisha wasafirishaji wanaokikuka sheria za nchi”.
Awali
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA, Ahmed Kilima, amesema mamlaka hiyo
inazidi kusogeza karibu zaidi huduma zake kwa wananchi kwa kufungua
ofisi zake katika mikoa 23 hadi hivi sasa.
Amesema malengo ya kufungua ofisi hizo ni kuimarisha shughuli za usimamizi na udhibiti wa usafiri katika mikoa husika.
Kilima
ametaja badhi ya majukumu ya ofisi hizo za mkoa ni kutoa na kuendeleza
lesani za usafirishaji abiria na mizigo, na kufuatilia utekelezaji wa
sheria, kanuni na taratibu za utoaji huduma za usafiri.
“Pia
zitashughulikia migogoro na malalamiko ya watoa huduma na watumiaji wa
huduma za usafiri na kuelimisha wadau na umma kwa ujumla juu ya majukumu
ya SUMATRA”,amesema Kilima.
EmoticonEmoticon