Kampuni ya Issere Sports yazawadiwa
Naibu
Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Amos Makala ambaye kwa sasa
amehamishiwa Wizara ya Maji kama Naibu Waziri akimkabidhi vyeti vya
utendaji bora wa huduma za michezo Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya
Issere Sports, Abbas Ally Issere katika kongamano la Wasanii
lililoandaliwa na Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Makala kwa sasa
amehamishiwa Wizara ya Maji kama Naibu Waziri (Picha na Mpiga Picha
Wetu).
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI
ya Issere Sports inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa vya michezo
nchini ni miongoni mwa wanamichezo, wasanii na awaandishi wa habari
1,000 waliotunukiwa vyeti vya utendaji bora katika fani za michezo kwa
mwaka 2013 hadi 2014 katika kongamano lililofanyika ukumbi wa Lamada,
Ilala Dar es Salaam.
Katika
kongamano hilo ambalo kulitolewa mada mbili za kusaidia jamii ya
wanamichezo kujiepuka na matumkizi ya dawa za kulevya, ya pili ikiwa ya
maadili bora katika jamii, Kampuni ya Issere ni pekee iliyopata nafasi
ya kuwakilisha nyingine zinazojihusisha na uuzaji wa vifaaq vya michezo.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Issere Sports, Abbas Issere aliyepokea vyeti hivyo kwa
niaba ya wanamichezo wengine wa Kampuni hiyo alisema zawadi hiyo ni
changamoto kwa wanamichezo kushirikiana pamoja badala ya kubaguana ili
kurejesha heshima katika michezo kama ilivyokuwa miaka ya zamani na
kutoa mfano kuwa katika riadha ilitawaliwa na Selemani Nyambui, Juma
Ikangaa na Filbert bayi.
Kampuni
ya Issere Sports ambayo imeingia mkataba wa kuuza jezi za Klabu ya
Simba, imekuwa ikiuza na kusambaza jezi hizo nchini na Mashirika ya
Umma, Wizara, Halmashauri za Wilaya na mashuleni katika ngazi ya shule
za msingi, Sekondari na vyuoni.
EmoticonEmoticon