DKT MREMA AMKINGIA KIFUA KIKWETE

January 21, 2014

Na Mwandishi Wetu, Moshi
 MBUNGE wa jimbo la Vunjo, Dkt Agustino Lyatonga Mrema, amewaonya  baadhi ya wanasiasa ambao  wamekuwa wakieneza siasa chafu  za  kubeza shughuli zinazofanywa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete,  kwa kushirikiana na Mbungu huyo,  katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Kauli hiyo ameitoa  juzi  wakati alipokuwa akiongea katika mkutano wake na  wananchi wa kata ya Himo- Makuyuni, wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, ambapo alisema Rais Kikwete  ameweza kufanya mambo makubwa katika jimbo hilo.


Alisema kazi ya wapinzani si kila kitu kupinga kazi ambazo zimekuwa zikifanywa na Mbunge, wanachopaswa ni kupongeza na kutoa ushauri pale ambapo wanaona kuwa hapajatekelezwa.



Dkt Mrema alisema moja ya kazi kubwa aliyoifanya Kikwete ni pamoja na kuwajengea barabara ya lami kutoka Marangu  mtoni hadi kilema Kusini yenye kilometa 5, ujenzi wa barabara ya Kwawawa hadi Nduoni Kirua vunjo yenye kilometa 10.

Dkt.Mrema na JK katika moja ya shughuli zilizokutanisha viongozi hao

Dkt Merema alisema kuwa Rais Kikwete  ameweza kusaidia  kutoa kiasi cha Shilingi milioni 150 kwa lengo la upatikanaji wa maji Safi na Salama katika  Mji wa Himo.

Aidha aliongeza kusema kuwa katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo ya kiuchumi pia Kikwete amewezesha masoko mawili ya Kimataifa, ambapo  soko la Lokolova litakuwa la nafaka na viwanda huku soko la Njia panda litakuwa la ndizi na mbogamboga.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »