![]() |
Marehemu Clement Mabina. |
MAZISHI ya aliyekuwa mwenyekiti
wa CCM na Diwani wa Kata ya Kisesa wilayani Magu Clement Mabina,
aliyeuawa kikatili na kundi la wananchi, yanatarajiwa kufanyika
Alhamisi.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa familia ya marehemu Mabina, Timothy
Gregory ambaye ni mdogo wa marehemu, alisema kwamba, mipango ya mazishi
imekamilika na zaidi ni pamoja na kusubilia mtoto wa kike wa marehemu
aliyoko njiani kutokea nchini Uingereza marehemu waliokuwa nje ya nchi.
Gregory alisema, Kijana mdogo wa marehemu (mtoto ) tayari amewasili jana
jioni, hivyo mazishi marehemu Mabina yatafanyika kesho kutwa Kisesa
wilayani Magu baada ya mtoto wake mkubwa wa kike kuwasili kutoka
Uingereza.
Mwenyekiti wa Kamati ya mazishi hayo, Henry Matata ambaye ni Meya wa
Manispaa ya Ilemela, amesema kuwa, taratibu za maziko ya marehemu
Mabina, zinaendelea kufanyika nyumbani kwa marehemu na kupokea wageni
mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara, wanasiasa wa Kada mbalimbali kutoka
vyama vya siasa na serikali pamoja na ndugu na rafiki wa karibu na
marehemu wa sehemu tofauti nchini kote na nje ya nchi za Jumuiya ya
Afrika Mashariki.
“Marehemu Mabina atazikwa rasmi Alhamisi saa 7:00 mchana katika shamba
lake kulekule Kitongoji cha Kanyama alikouawa. Tayari tumerudisha
mabango ya kuzuia watu waliokuwa wakichimba mawe na mchanga kwenye eneo
hilo, yaliyoondolewa na kundi la watu waliomshambulia na majirani
wamepokea na kudai eneo hilo lilikuwa likimilikiwa na marehemu kihalali
kwani serikali ya kijiji ililikabidhi kwa marehemu kupitia mkutano wa
hadhara hali iliyodaiwa kumuua ilikuwa kumuonea na ilitawaliwa na siasa
zaidi kuliko uhalisia wa madai ya kundi la watu hao wachache .” alidai
Matata.
Hadi sasa, mamia ya waombolezaji wakiwemo ndugu, jamaa, wananchi wa
Kisesa, wana CCM na viongozi mbalimbali wa Chama na serikali walikuwa
wakiendelea kumiminika nyumbani hapo kuomboleza.
Nacho Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza, Mwenyekiti wa CCM wa mkoa
wa Mwanza, Anthony Diallo kimetoa pole kwa wananchi wa Kisesa wakiwemo
ndugu na jamaa wa familia za marehemu Mabina na mtoto Temeli Malimi
(12) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na marehemu huyo wakati wa
purukushani za kujiokoa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Magu, Desidery Kiswaga alisema
kwamba, marehemu Mabina aliyekuwa Mweneykiti wa zamani wa CCM mkoa wa
Mwanza, atazikwa kwa heshima zote stahili.
EmoticonEmoticon