Na Twahiru Mdimu ,Dodoma.
MASHINDANO ya Shirikisho
za Serikali za Mitaa(Shimisemita) yanayoendelea kutimua vumbi mkoani Dodoma yameingia hatua ya
robo fainali huku timu kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga zikiendelea kufanya
vizuri katika mashindano hayo.
Timu za Halmashauri ya
Jiji la Tanga kutokana na kufanya vizuri katika mashindano hayo leo
zimefanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ambapo mechi hizo zitaanza majira ya
saa nane mchana.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizoifikia blog ya Tanga Raha zimeeleza kuwa timu ya Halmashauri ya Jiji la
Tanga leo jioni itakuwa na kibarua kizito kuweza kuwakabili timu ya Halmashauri ya Mtwara
Mikindani kwenye mchezo wa mpira wa miguu.
Katika mchezo mwengine
unaotarajiwa kuwa na upinzani wa hali ya juu ni wa pete ambapo timu ya Halmashauri
ya Jiji la Tanga watakapowakabiliana wenzao kutoka Halmashauri ya wilaya ya
Kyela.
Licha ya kuchezwa mchezo
huo kutakuwa na mechi nyengine ambayo itachezwa saa kumi jioni Halmashauri ya
wilaya ya Kinondoni watacheza na Halmashauri ya wilaya ya Ulanga kwenye michezo
ambao unatazamiwa kuwa na upinzani mkubwa.
EmoticonEmoticon