Na Oscar Assenga,Tanga.
MKUU wa wilaya ya
Tanga,Halima Dendego anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Ligi ya
Umoja wa Vijana kata ya Mabawa (UVCCM)itakayoanza kutimua vumbi Jumapili wiki
hii kwenye viwanja wa soka Mikanjuni Sekondari.
Akizungumza
leo,Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Mabawa, Ramadhani Hanaph alisema maandalizi ya
kuelekea mashindano hayo yanaendelea vizuri na kinachosubiriwa ni kuanza kwake.
Hanaph alisema mashindano
hayo yatashirikisha timu kumi na tatu ambazo zitagawanywa katika makundi mawili
ambayo itachezwa kwa mfumo wa ligi.
Alisema mashindano hayo
yatafunguliwa Jumapili kuanza majira ya saa tisa mchana ambapo zitaanza
shamrashamra kwa timu zote kumi na tatu kujipanga kwenye mstari ili kusubiri
kukaguliwa na mgeni rasmi.
Mwenyekiti huyo alisema
lengo la mashindano hayo ni kuinua vipaji katika kata hiyo na kuhamasisha
vijana kupenga michezo na kujiepusha kutumia madawa ya kulevya.
EmoticonEmoticon