JIJI TANGA WAENDELEA KUNYANYASA SHIMISEMITA DODOMA.

November 01, 2013


Na Twahiru Mdimu,Dodoma. 

TIMU ya Mpira wa Miguu ya Halmashauri ya Jiji la Tanga leo Imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Serikali za Mitaa nchini (Shimisemita)baada ya kuibamiza Mtwara Mikindani mabao 2-0,kwenye mchezo wa robo fainali uliochezwa dimba la Jamhuri mkoani Dodoma.

Mchezo huo ambao ulikuwa wa aina yake huku timu ya Halmashauri ya Jiji la Tanga ikionekana kuutawala kipindi cha kwanza na cha pili kwa kucheza kwa umakini mkubwa na kufanikiwa kuandika bao lao la kwanza ambalo lilifungwa na Ibrahim Mustapha katika dakika ya 8.

Mpaka timu zote zinakwenda mapumziko,Halmashauri ya Jiji la Tanga ilikuwa ikiongoza katika mchezo huo ambapo kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikionekana kujipanga vema .

Wakionekana kucheza kwa umakini na umahiri mkubwa Halmashauri ya Jiji la Tanga waliweza kupeleka mashambulizi mara kwa mara langoni mwa Mtwara Mikindani na kufanikiwa kupata bao lao la pili kwenye dakika ya 80 ambalo lilifungwa nyota wa mchezo huo Ibrahim Mustapha.

Akizungumza na Tanga Raha mara baada ya kumalizika mchezo huo,Mweka Hazina wa timu ya Jiji la Tanga,Twahiru Mdimu aliwapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kuendelea kulipa heshima jiji hili kwa kufanya vizuri kwenye michezo yao wanayokuwa wakicheza.

Licha ya kuwapongeza wachezaji hao ,aliwataka kuhakikisha wanaendelea kuilinda heshima ya jiji la Tanga kwa kufanya vizuri kwenye mechi yao ya nusu fainali ambayo itachezwa kesho kati yao na timu ya Kyela.

Akizungumzia hali za wachezaji wa timu ya Tanga,Mdimu alisema wanaendelea vizuri isipokuwa wachezaji wawili ambao wamepata majeraha katika mechi yao ya leo ambapo ni Daudi Kiweri.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »