Kamishna wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja akabidhi vyeti vya udereva kwa mafunzo ya maaskari magereza

November 02, 2013
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(mbele katika Jukwaa) akipokea Saalam ya heshima na Utii kutoka kwa Gadi Maalum ya Gwaride lililoandaliwa na Wahitimu 72 wa Mafunzo Maalum ya Udereva katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva Kingolwira, kilichopo Mkoani Morogoro. Hafla fupi ya ufungaji Mafunzo hayo imefanyika leo Novemba 1, 2013 katika viwanja vya Kingolwira, Morogoro.

Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja  (kulia) akikagua Gadi Maalum ya Gwaride lililoandaliwa Maalum kwa ajili ya Ufungaji Mafunzo ya Udereva Kozi No. 19 ya Mwaka 2013 ambayo yamefanyika leo Novemba 1, 2013 katika Chuo cha Magereza cha Ufundi na Udereva Kingolwira, Mkoani Morogoro.


Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja akimkabidhi cheti mmoja wa Wahitimu wa Kozi ya Udereva, Cpl. Nuru kutoka Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Dar es Salaam. Cpl. Nuru ni minongoni mwa askari 11 wa Kike ambao wamehitimu mafunzo Maalum ya Udereva leo Novemba 1, 2013  na Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa Mwezi mmoja katika Chuo cha Ufundi na Udereva Kingolwira, Mkoani Morogoro ambapo jumla ya Askari 72 wamehitimu Mafunzo hao kwa ustadi mkubwa.

Picha na Kambi Mbwana wa Handenikwetublog.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »