Na Oscar Assenga, Tanga.
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Coastal
Union ya Tanga, Albert Clement Peter “Mkubwa wa Kazi amekanusha vikali taarifa
zilizosambazwa na baadhi vyombo vya habari kuwa wamemfukuza kocha wao mkuu
Hemed Morroco.
Akizungumza na Blog hii, Peter alisema wao hawajamfukuza
kocha huyo kama ilivyoripotiwa bali mkataba wake wa kuendelea kuinoa timu hiyo
umekwisha hivyo wataangalia hatima yake kama watamuongezea au la.
Alisema hivi sasa kocha huyo yupo mjini Bukoba akiwa
na kikosi cha timu hiyo wakijiandaa na mechi yao dhidi ya Kagera Sugar ambayo
itachezwa Jumamosi hii kwenye dimba la soka la Kaitaba.
“Mimi
nashangaa sana kusikia baadhi ya vyombo vikiripoti tumemfukuza Morroco hizo
habari wamezitoa wapi jamani acheni uzushi Morroco bado ni kocha wetu na yupo
na timu bukoba “Alisema Peter.
Mjumbe huyo alisema uongozi wa klabu hiyo
umeshapitisha jina la msemaji wao na hivyo wanatarajia kumtangaza muda wowote
ambaye atachukua nafasi ya Edo Kumwembe.
Alisema mkataba wa kocha huyo uliisha tokea mwanzoni
mwa mwezi huu ambapo bado uongozi haujakaa naye na kuzungumza kuhusiana na
mkataba mpya.

EmoticonEmoticon