WAKULIMA WA KOROSHO KATA YA BWITI MKINGA WAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA ZA KUKAMILISHA MALIPO.

August 12, 2013

NA OSCAR ASSENGA,MKINGA
WAKULIMA wa Korosho wa Kata ya Bwiti wilayani Mkinga wameitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kukamilisha malipo ya  korosho ili kuondoa uwezekano wa kutokea vitendo vya uvunjifu wa amani kama ilivyokuwa kwa wananchi wa Mtwara.

Wananchi hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakizungushwa kuhusu malipo stahili ya korosho zao na kumpa siku tatu Diwani wa Kata hiyo, Peter Kimweri kuhakikisha wanalipwa fedha hizo.

Wamesema ni jambo la kushangaza kuona hadi sasa bado hawajalipwa fedha zao za korosho huku kukiwa hakuna taarifa yoyote kutoka Serikalini.

Akizungumza na blogg hii,Diwani wa Kata hiyo, Kimweri amekiri kuwepo kwa malalamiko hayo ya wakulima na kumtaka Mkuu wa wilaya ya Mkinga kuingilia kati ili kunusuru kutokea vitendo vya uvunjifu wa amani.

Kimweri amesema kwa muda mrefu wakulima hao wamekuwa wakilalamikia fedha zao na kwamba Serikali imekuwa kimya hali inayopandikiza chuki miongoni mwa wakulima dhidi ya Serikali yao.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »