EWURA YAENDELEA KUTOA ELIMU KWENYE MAONESHO SABASABA

July 02, 2025
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu yake na namna ya kushiriki katika ufuatiliaji wa huduma za nishati na maji nchini, kupitia ushiriki wake kwenye Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.

EWURA imetumia jukwaa hilo kubwa la kitaifa na kimataifa kuonesha namna inavyosimamia sekta za umeme, mafuta ya petroli, gesi asilia na maji safi na usafi wa mazingira sambamba na kutoa elimu kwa umma kuhusu haki na wajibu wa watumiaji wa huduma hizo.

Maonesho ya Sabasaba ya mwaka huu yamewakutanisha taasisi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo EWURA ni miongoni mwa taasisi zinazotoa huduma za moja kwa moja kwa wananchi kwa lengo la kuboresha maisha yao na mazingira ya biashara nchini.

Wananchi wametakiwa kutembelea banda la EWURA katika viwanja vya Sabasaba, kujipatia elimu, kuwasilisha hoja au malalamiko na kupata machapisho mbalimbali yanayoelezea kazi za Mamlaka hiyo.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »