MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT)Sophia Simba amewataka wanachama ndani ya umoja huo kuvunja makundi yaliopo miongoni mwao na waelekeze nguvu zao katika kutimiza majukumu yao lengo likiwa ni kuimarisha umoja huo.
Simba ambaye pia ni Waziri wa Jinsi na Watoto alitoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo kwa viongozi na watendaji wa UWT kanda ya kaskazini iliyokuwa na malengo ya mpango mkakati wa kutekeleza majukumu yao ya kila siku yaliyofanyika katika ukumbi wa CCM Hall mkoani Tanga.
Licha ya kuzungumzia suala hilo lakini pia watakuwa na mikakati ya UWT katika kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015 ambapo amewataka makatibu wa umoja huo ngazi ya chini kuhakikisha wanakuwa karibu na wanachama wao na kuacha tabia ya kuwapigia simu na kuwauliza maswali ya kuwa leo kuna mkutano au la.
Aidha aliwataka makatibu hao kubadilika na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani viongozi wanapaswa kujinyenyekeza na kwenda vijiji lengo likiwa ni kusukuma gurudumu la maendeleo kwenye maeneo yao pamoja na kuupa nguvu umoja huo.
Waziri Simba amewataka makatibu na wenyeviti kuwa wapo kwenye wakati mgumu sana hivyo wasigawanyike na kueleza akigundua viongozi wenye tabia kama hiyo hawatawavumilia badala yake wataondolewa kwani viongozi wa namna hiyo watashindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Aidha amewataka UWT kuwa wakakamavu ili kuweza kuuimarisha umoja huo ikiwemo kuwa karibu na wakina mama ili uweza kuweza kuwasikiliza shida zao pamoja na kuwatetea pale wanapoona wakionewa katika jamii zao zinazowazunguka.

EmoticonEmoticon