MWANA FA AHAMASISHA WAPIGA KURA WAJITOKEZE KUJIANDIKISHA

February 13, 2025



📌 Ni daftari la Kudumu la wapiga kura zoezi linaanza Leo


📌 Awasihi wasijiandikishe mara mbili kukwepa rungu la kisheria


MBUNGE wa Jimbo la Muheza Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA  amewataka wakazi wa wilaya ya Muheza, kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la Kudumu la wapiga kura lililoanza leo.


MwanaFA ambaye ni Naibu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, alisema zoezi la undikishaji wapiga kura umeanza leo (Februari 13) na litafanyika kwa siku Saba hadi Februari 19 litamalizika.


Aliomba wadau wilayani Muheza, wakiwemo viongozi wa dini,  kuwahamasisha watu wenye sifa kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari hilo.


"Kufanikiwa kwa uboreshaji wa daftari hili kunategemea sana wadau kutoa elimu ili watu wenye sifa wajitokeze kwa wingi wakaandikishwe au kuhamisha, kuboresha taarifa zao," alisema MwanaFA.


Hata hivyo, mbunge huyo aliwasihi wananchi wasijiandikishe mara mbili ili wakwepe kukumbana na Sheria.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »