WANANCHI TANGA, PWANI WAITIKIA VYEMA UBORESHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

February 13, 2025

 

Mpiga Kura Bi. Habiba Kingazi mkazi wa Mtaa wa Lumumba, Kata ya Ngamiani Kaskazini akionesha kadi yake baada ya kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na kupatiwa kadi mpya katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji TADECO ,Halmashauri ya Jiji la Tanga.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akishuhudia mwananchi akiboresha taarifa zake.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akimkabidhi kadi ya mpya ya Mpiga Kura Bi. Habiba Kingazi mkazi wa Mtaa wa Lumumba, Kata ya Ngamiani Kaskazini aliyeboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura na kupatiwa kadi mpya katika kituo cha Ofisi ya Mtendaji TADECO ,Halmashauri ya Jiji la Tanga.  Zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa mikoa ya Tanga na Pwani limeanza leo leo Februari 13 hadi 19, 2025 na litadumu kwa siku saba.
******************** 
Na. Waandishi Wetu, Tanga
Wananchi wa mikoa ya Tanga na Pwani leo Februari 13, 2025 wameanza uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo wananchi wengi wamejitokeza kushiriki katika zoezi hilo.
 
Mwandishi wa Habari hizi aliyeambatana na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele Mkoani Tanga walishuhudia watu wengi wakiwa katika foleni kutimiza haki yao hiyo ya kikatiba ya kujiandikisha kuwa Wapiga Kura.
 
Aidha akizungumza baada ya kutembelea vituo katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Jiji la Tanga, Mhe. Jaji Mwambegele alisema zoezi hilo limeanza vizuri na hakuna changamoto ya vifaa wala watendaji.
 
“Nilianza kushuhudia tangu kufunguliwa kwa kituo majira ya Saa 2:00 asubuhi pale katika kituo cha Ofisi ya Mtedaji TADECO kilichopo mtaa wa Lumumba Kata ya Ngamiani Kaskazini, na kushudia zoezi likienda vizuri pasipo kuwa na changamoto zozote,” alisema Mhe. Jaji Mwambegele.
 
Alisema baadhi ya wananchi waliojitokeza walikua wanataka tu kuwa na kadi mpya za Mpiga kura lakini kadi zao za awali hazikua nachangamoto yeyote hivyo akatoa ushauri kwa Waandishi Wasaidizi vituoni kuwa wawaulize watu kabla ya kuwaandikisha.
 
“Kuna baadhi ya wananchi wamekuja kwaajili ya kupata vitambulisho vipya, lakini vitambulisho vya awali havina tatizo lolote, hivyo, Nimesisitiza wananchi wakifika vituoni waulizwe kwanza na kueleweshwa,” alisema Mhe.Jaji Mwambegele.
 
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kutumia fursa hiyo ya kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika siku za mwanzo na wasisubiri siku za mwisho kwani siku saba si nyingi.
 
Baadhi ya Wananchi waliozungumza na Mwandishi wetu, akiwepo Abubakar Ally, Mwanaharusi Moyo , Bakari Salim Kibamba na Mwl. Taji Walter Mussa ambao ni wakazi wa Jiji la Tanga waliishukuru Tume kwa kuendesha zoezi hilo.
 
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika uanaofanyika katika mikoa Tanga na Pwani kwa siku saba kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari, 2025 unataraji kuandikisha Wapiga Kura wapya 431,016 na zoezi hilo litakapokamilika mikoa hiyo itakuwa na wapiga kura 2,727,318.
 
Tanga itatekeleza zoezi hilo kwa awamu mbili ambapo kwa sasa zoezi linafanyika katika  Halmashauri ya Jiji la Tanga, Halmashauri za Miji ya Handeni na Korogwe na Halmashauri za Wilaya ya Kilindi, Lushoto na Muheza.
 
 Wakati wa Mkutano wa Tume na Wadau mkoani Tanga,  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Ndugu. Kailima R.K alisema,  Tume imeshakamilisha zoezi hilo kwenye mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma, Singida, Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe, Ruvuma Lindi na Mtwara.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akishuhudia mwananchi akiboresha taarifa zake.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akishuhudia mwananchi wa Mtaa wa Lumumba, Kata ya Ngamiani Kaskazini aliyekuja kujiandikisha akichukuliwa picha wakati alipotembelea kituo cha Ofisi ya Mtendaji TADECO katika Halmashauri ya Jiji la Tanga kushuhudia mwenendo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambalo limeanza leo uboreshaji katika mikoa ya Tanga na Pwani. Zoezi hilo litadumu kwa siku saba kuanzaia leo Februari 13 hadi 19, 2025. 

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akitazama kitambulisho kikitoka katika Printa.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza na mawakala wa vyama. 
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akishuhudia wananchi wakiwa katika foleni kusubiri kuboresha taarifa zao. 

Mkazi wa Tanga katika Kata ya Mabawa akisoma bango la maelezo. 

Wananchi wakiendelea kuajindikisha na kuboresha Taarifa zao Jijini Tanga.
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Jaji wa Mahakama Kuu, Mhe. Asina Omari leo tarehe 13 Februari 2025 ametembelea baadhi ya vituo vya kuandikishia wapiga kura vilivyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani na kushuhudia wananchi wakiendelea kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri leo tarehe 13 Februari 2025 ametembelea baadhi ya vituo vya kuandikishia wapiga kura vilivyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani na kushuhudia wananchi wakiendelea kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Magdalena Rwebangira, ametembelea vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, vilivyopo katka Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga leo tarehe 13 Februari, 2025.

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »