ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA SHERIA

February 11, 2025

 Na Rahma Khamis Maelezo


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuweka misingi Bora ya Haki ili wananchi kupata haki zao.

Ameyasema hayo Uwanja wa Mahakama ya Mkoa Mazizini Wilaya ya Magharibi ‘B' katika kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Sheria.

Amesema uwepo wa Sheria na upatikanaji wa Haki ni jambo muhimu kwani itawawezesha wananchi kupata mafanikio

Rais Mwinyi amezisisitiza mahkama kutumia maadili katika kazi zao ili wananchi wapate nafasi ya kusema yale waliyonayo.

Aidha amesema kuwa maboresho ya Sheria lazima yaende sambamba na upatikanaji wa haki kwa wakati hivyo ni vyema kuweka utaratibu mzuri na mwepesi ili kuwarahisishia wananchi.

Nae Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Dkt Haruon Ali Suleiman amewataka majaji na mahakimu kujitahidi katika utendaji wa kazi zao ili kesi zisichukue muda mrefu.

Akitoa salamu Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla amesema kufanyika kwa maadhimisho hayo kunaashiria kumalizika kwa mapumziko ya mahakama na kuukaribisha mwaka mpya wa shughuli za mahakama.

Amesema kuwa maadhimisho hayo kwa Zanzibar ni ya kumi na nne ambapo Kauli mbiu yake inaunga mkono uimarishaji wa misingi ya haki na sheria pamoja na kuitaka jamii na Taasisi mbali mbali kufahamu kuwa mahakama ndio kimbilio la upatikanaji wa Haki.

Aidha amefahamisha kuwa kwa mwaka 2024 vikao 224 vilifanyika na kushirikisha Watendaji mbalimbali ikiwemo Mkemia Mkuu wa Serikali, Afisi ya Mwanansheria Mkuu pamoja na utungaji wa Sheria ya mahakama ya mwaka 2023 ya mahkama ya kadhi ili kurahisisha upatikanaji wa Haki.

Mwanansheria Mkuu wa Zanzibar Mwinyi Talib Haji ameipongeza Serikali ya awamu ya nane kwa kuweka na kuimarisha miundombinu ya Sheria kwa kuweka misingi imara ya upatikanaji wa ikiwemo vitendea kazi na watendaji wake.

Aidha amefahamisha kuwa Afisi imekamilisha mapitio ya Sheria mpya hivyo itarahisisha upatikanaji wa Sheria pamoja na kukamilisha rasimu ya Sheria na baadae kupitisha katika Baraza la Wawakilishi.

Maadhimisho ya Sheria hufanyika kila mwaka ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu Utawala wa Sheria ndio Msingi wa Haki,Amani na maendeleo katika jamii.

























Share this

Related Posts

Previous
Next Post »