Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom
Tanzania, Gregory Verbond (kulia) na Mkurugenzi Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga
(TTCL), Reinhardt Swart (kushoto) wakiwekea makubaliano ya mteja kunua saruji kwa M PESA bila tozo yoyote popote nchini.
Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) na Mkurugenzi kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Tanga (TTCL), Reinhardt (kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano ya mteja kununua Saruji kwa M PESA bila tozo yoyote popote nchini.
Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond (kulia) akizungumza mara baada makubaliano na kiwanda cha Saruji cha Simba Cement kwa mteja kununua Saruji kwa M PESA bila tozo popote nchini.
Mmoja wa wakala wa Simba Cement Tanga, Athuman Ali (kulia) alievaa kibagalashia akiwa mmoja wa watu waliohudhuria makubaliano ya utiaji saini wa Ununuaji wa Saruji kwa M PESA baina ya Kampuni ya Vodacom Tanzania na Kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga leo.
William Mgazija wa ITV aliesimama nyuma na kushika MIC ni miongoni mwa wahudhuriaji wa makubaliano ya utilianaji wa saini wa manunuzi ya Saruji kwa M PESSA
Waandishi wa habari nao walikuwa miongoni mwa waalikwa wa ushuhudiaji wa utilianaji saini makubaliano ya ununuzi wa Saruji kwa M PESA. Kutoka kushoto alievaa Ushungi ni Amina Omari wa Gazeti la Mtanzania , Betha Mwambellah wa TBC na Maryam Mwandishi wa Jambo leo
KIWANDA
Cha Saruji cha Simba Cement (TCCL) cha Tanga, kimeinmgia makubaliano na Kampuni ya
simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania Limited, kwa mteja kununua saruji kwa
kutumia M PESA bila tozo yoyote.
Makubaliano hayo yaliyofanyika leo
viwanja vya Hotel ya Tanga Beach na kushuhudiwa na viongozi wa pande zote mbili
na kutajwa kuwa yatakuwa mkombozi kwa mwananchi wa kipato cha chini kwa kununua
Saruji kwa simu badala ya kutumia Taasisi za pesa na kupanga foleni.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Afisa Mkuu Biashara wa Vodacom Tanzania, Gregory Verbond, alisema kampuni yake
imechukua uamuzi huo wa makubaliano na kampuni ya Cement kwa lengo la kumsaidia
mwananchi wa kipato cha chini.
Alisema mteja ataweza kununua Saruji
(Simba Cement) kwa kutumia M PESA na hakutakuwa
na tofati ya mnunuzi wa mifuko mingi na michache ambapo hatotozwa ada yoyote
mnunuaji.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa
kiwanda cha Saruji, Simba Cement, Renhardt Swart, alisema makubaliano hayo ni
moja ya sera za kiwanda kumsaidia mwananchi wa chini kuweza kukabiliana na
changamoto za maisha.
Alisema Kiwanda cha Simba Cement
daima kiko kwa ajili ya wananchi na faida inayopata inairejesha kwa wananchi na
kuwataka kuitumia fursa hiyo ambayo iko na unafuu kwa ununuaji.
Habari kwa Hisani ya Tanga Kumekucha Blog
EmoticonEmoticon