Showing posts with label siasa. Show all posts
Showing posts with label siasa. Show all posts

DC SUMAYE AONGOZA WANANCHI KUPIGA KURA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

November 27, 2024 Add Comment

 

 

Na Ashrack Miraji 

Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Zephaniel Sumaye, leo tarehe 27 ameongoza wananchi katika zoezi la kupiga kura la uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo wanachagua viongozi wa Serikali ya Mtaa, kitongoji na vijiji katika kituo cha Chake Chake, kilichopo wilayani Lushoto, mkoani Tanga.

Akizungumza baada ya kupiga kura, Mhe. Sumaye aliwashukuru wananchi wa wilaya ya Lushoto kwa ukomavu wao wa kisiasa na kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo, akieleza kuwa ni ishara ya maendeleo katika demokrasia. Aliwataka wananchi kuendelea kushiriki kwa wingi ili kuchagua viongozi wanaowataka, huku akisisitiza kuwa zoezi hilo linatakiwa kuwa la amani na utulivu.

“Tunashuhudia ukomavu mkubwa wa kisiasa kutoka kwa wananchi wa wilaya ya Lushoto. Kampeni zilifanyika kwa amani na hakuna malalamiko kutoka kwa vyama au wagombea,” alisema Mhe. Sumaye. “Ninawaomba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi ili kuhakikisha wanachagua viongozi bora watakaowaongoza katika maendeleo ya jamii yetu.”

Mhe. Sumaye pia aliwasisitizia vyama vya siasa na wanachama wao kuheshimu kanuni za uchaguzi, akieleza kuwa malalamiko yoyote kuhusu uchaguzi yanapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na Tume ya Uchaguzi.

Aidha, Mhe. Sumaye aliwataka wananchi kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima wakati wa uchaguzi, akiwataka waendelee na shughuli zao  baada ya kupiga kura, ili kuepuka msongamano na usumbufu. na Alisisitiza kuwa hii ni siku ya mapumziko iliyotengwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili wananchi waweze kushiriki kwa wingi katika uchaguzi.

Kwa upande mwingine, Dkt. Ikupa Mwaysoge, Msimamizi  wa Uchaguzi wilaya ya Lushoto, alisema vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema asubuhi na hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza hadi sasa. Alisema wananchi wamejitokeza kwa wingi na hali ni shwari katika maeneo yote ya uchaguzi.

“Tunawashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi. Hii ni fursa muhimu ya kutimiza wajibu wa kikatiba, kuchagua viongozi bora watakaoweza kuleta maendeleo kwa jamii,” alisema Dkt. Mwaysoge.

Linoss Mwita, mkazi wa Lushoto, ambaye ni kijana, alisema kuwa aliona ni muhimu kushiriki katika uchaguzi huu, kwani ni haki yake ya kikatiba. Alisema kuwa ili kupata viongozi bora, ni lazima wananchi wawe na ushiriki mkubwa katika mchakato wa uchaguzi.

“Leo ni siku ya kupumzika, kama alivyosema Rais wetu, hivyo tunatumia siku hii kutekeleza wajibu wetu wa kikatiba. Napenda kuwahimiza vijana wengine kujitokeza kwa wingi ili kuchagua viongozi bora,” alisema Mwita.

Kauli mbiu ya uchaguzi wa mwaka huu ni: “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi.”




 

TAYARI NIMEPIGA KURA,WEWE JE?

November 27, 2024 Add Comment




Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Wakili Stephen Byabato leo Tarehe 27 Novemba 2024 amepiga kura kuwachagua Viongozi wa Serikali za Mitaa katika kituo cha Chuo Huria Mtaa wa Migera - Nshambya Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera.

NIMEPIGA KURA NIMETIMIZA HAKI YANGU YA KIKATIBA-MHE KAPINGA

November 27, 2024 Add Comment



📌 *Aungana na Wananchi kuchagua Viongozi Kitongoji cha Mheza*


📌 *Ahimiza Watanzania kuendelea kujitokeza kupiga kura*


Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga leo ameshiriki zoezi la kupiga

kura katika Kitongoji cha Mheza kijiji cha Mkumbi Halmashauri ya Mbinga Vijijini ili kuchagua viongozi wa eneo husika.



Kapinga ameeleza kuwa, kwa kufanya hivyo ametimiza haki yake ya kikatiba na kutoa wito kwa Watanzania wote kuitumia haki hiyo kikamilifu.



Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni miongoni mwa mihimili muhimu ya Demokrasia inayowezesha ushiriki wa wananchi katika uongozi wa maeneo yao.




NLD YAHIMITISHA KAMPENI KWA KISHINDO HANDENI YAWAOMBA WANANCHI KUWAPA RIDHAA WAGOMBEA WAO ILI WAWAPE MAENDELEO

November 26, 2024 Add Comment


Na Oscar Assenga,HANDENI.

CHAMA cha The National League For Democracy (NLD) kimehitimisha kampeni kwa wagombea ambao wanawania nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu huku wakiwawataka wananchi kuwapa ridhaa ili waweze kuwapa maendeleo.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kampeni wa kuhitimisha kampeni hizo katika viwanja vya soko la Misima wilayani Handeni,Katibu Mkuu wa NLD Doyo Hassani Doyo alisema kwamba chama hicho kimejipanga kuhakikisha wanatatua kero za wananchi zinazowakabili kwa muda mrefu.

Alisema kwamba wagombea ambao wamewasimamisha kwenye maeneo yote wanauwezo mkubwa wa kuweza kuwatumikia wananchi na kuwasaidia kutatua changamoto ambazo zinawakabili kutokana na kwamba wanatosha na uwezo wa kuwaongoza.

“Sisi katika uchaguzi huu tumewasimamisha wagombea wasiokuwa na njaa lakini pia wenye uwezo wa kutoa ajira kwa wengine kupitia fursa tulizonazo na wengi wametoa ajira kwenye jamii zinazowazunguka”Alisema

Awali akizungumza Mwenyekiti wa NLD wilaya ya Handeni Rajabu Doyo aliitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kufanya uchunguzi haraka iwezekanavyo kwa baadhi ya wagombea wa vyama vya siasa kuandika barua za kujitoa kwenye uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa.

“Haiwezekani mgombea anachukua fomu ya kugombea anaijaza halafu akairudisha alafu leo unaambiwa kajitoa hii ni rushwa ya wazi wazi kabisa kwa hiyo tunaiomba Takukuru iingilie kati haraka iwezekanavyo “Alisema

Mwisho.

HATUNA HURUMA TUNABEBA VYOTE -DKT.BITEKO

November 25, 2024 Add Comment




📌 *Tunataka Tuoneshe Afrika na Dunia Tanzania ni Nchi ya Demokrasia*


📌 *Asema CCM Imejipanga Kushinda na Kuleta Maendeleo*


📌 *Asema CCM Inataka Ushindi wa Heshima*


Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa CCM chini ya uongozi wa Rais Samia imejipanga kuifanya Geita kuwa na maendeleo zaidi na katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaofanyika Novemba 27, 2024  wananchi waichague CCM na kuipa ushindi wa heshima.


Ametolea mfano wa jitihada za kuiletea maendeleo zilizofanywa na CCM kuwa ni pamoja na juhudi za Rais Samia za kuhakikisha Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) unawanufaisha zaidi wananchi kwa Geita.


Dkt. Biteko amesema hayo  Novemba 24, 2024 wakati akihutubia katika Kampeni zinazoendelea za


Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Wilaya ya Geita zilizofanyika katika Viwanja vya Nyankumbu mkoani Geita.


“ Sasa tunaona miradi  mbalimbali ikitekelezwa, Geita maendeleo yapo kila kona tunataka mchague viongozi watakaoshirikiana na viongozi wengine ili kutuletea maendeleo, CCM tunataka ushindi wa heshima,” amesema Dkt. Biteko. 


Amesisitiza “ Kwetu sisi hivi ni vyama rafiki na Mhe. Rais anaeleza kuhusu falsafa ya 4R, tunataka tuiambie Afrika na dunia kuwa Tanzania ni nchi ya demokrasia na tunafuata misingi ya waasisi wetu na sisi  Geita hatuta wabagua vyama vingine lakini jambo moja hatuna huruma nalo ni kura na hatuwapi kura hata moja,” 


Ameongeza “ CCM tunabeba vyote, tunabeba vijiji, vitongiji na mitaa yote hatuwaachi hata kimoja na tunafanya  hivyo kwa sababu wananchi wameridhishwa na kazi kubwa ya miradi ambayo CCM  imetekeleza hapa na inaendelea kutekeleza.” 



Aidha, Dkt. Biteko amesema kuwa Serikali imefanya jitihada kubwa za kuhakikisha Tanzania inaendelea kuimarika kiuchumi kwa kuanzisha miradi ya umeme ambayo imeongeza utoshelevu wa umeme nchini pamoja na uwepo wa  treni ya umeme ambayo imeanza safari zake kutoka Dar es salaam hadi Dodoma na inatarajiwa kufika Burundi hapo baadae.


Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Mhe. Constantine Kanyasu amesema kuwa Wilaya ya Geita imejipanga kushinda katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kuwa wananchi wameona miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo.


Vilevile, Kanyasu ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya afya, elimu na barabara ambayo inaendelea vizuri.


Mbunge wa Jimbo la  Busanda, Mhe. Tumaini Magesa amewahimiza wananchi wa Geita kuwapigia kura wagombea wa CCM kwa kuwa Serikali ya Rais Samia ina nia ya dhati ya kuwaletea maendeleo.

 


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Geita, Muhoja Mapande amesema kuwa wilaya yake ina vijiji 158, mitaa 65 ambapo vyama vingine vimeweka wagombea 50 na nane kati yao hawataendelea kugombea, katika vitongoji 640 vyama vingine vimeweka wagombea 115 ambapo 92 kati yao wameandika barua ya kutoaendelea na vyama hivyo.


Ameendelea kusema  wagombea wa vyama hivyo wamefikia uamuzi huo baada ya kuona jitihada za CCM za kuleta maendeleo katika wilaya hiyo.


MWISHO