Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akishiriki UDS Marathon iliyoandaliwa kwa ajili ya kuboresha mazingira ya Wanafunzi chuoni hapo kushoto ni Rais Mstaafu awamu ya nne na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Jakaya Kikwete, Kulia ni Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa William Anangisye Jijini Dar es Salaam
WAZIRI DKT ASHATU KIJAJI MGENI RASMI MASHINDANO YA RIADHAA YA CLIMATE CHANGE 2024 PANGANI
michezoWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt Ashatu Kijaji anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya Riadhaa ya Climate Change 2024 yatakayofanyika wilayani Pangani kesho Novemba 30 mwaka huu.
Mashindano hayo yameandaliwa na Asasi ya Kiraia ya Tree Of Hope kwa kushiriana na Asasi nyengine za Mtandao wameandaa mbio hiyo fupi katika Mji Mkongwe wa Pangani na wageni kutoka maeneo mbalimbali Tanzania Bara na Visiwani watashiriki.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya ya Pangani Gift Msuya alisema maandalizi ya mbio hizo yamekamilika na yamefikia zaidi ya asilimia 90 ambapo wanatarajia Waziri Dkt Ashatu Kijaji kuwasili wilayani humo akiwemo Rais wa Chama cha Riadha nchini (RT) Anthony Mtaka,
Msuya alisema kwamba kwa upande wa njia ambazo zitatumika kwa wakimbiaji hao zipo katika hali nzuri na maeneo ya malazi yapo vizuri huku akisisitiza suala la ulinzi na usalama limeimarishwa kuhakikisha kila kitu kinafanyika kama kilivyopangwa.
Alitaja mbio ambazo zitakimbiwa na wakimbiaji kuwa ni zile zenye umbali wa Kilomita 21,Kilomita 10 na Kilomita 5 ambapo wakimbia wasiopungua 300 kutoka Tanzania Bara na Visiwani wanatarajiwa kushiriki mbio hizo.

Aidha aliwakaribisha wadau wote wa mbio na mazingira huku akieleza lengo lake ni kushirikisha wadau wa mazingira kuchangia upatikanjaji nishati safi ya kupikia ikiwa kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu ambaye ndie kinara wa matumizi ya nishati safi ya kupika katika Taifa ,Africa na Duniani .

Hata hivyo alisema kwamba wanatarijia kupata majiko ya gesi na nishati mbadala kwa kaya mbalimbali hasa zile ambazo hazijiwezi kutumia nishati safi kwa sababu ya kipato.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia ya Tree Of Hope Fortunata Manyeresa kwamba kupitia mbizo hizo wanakwenda kuleta hamasa mpya na kujenga uelewa wa jamii kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake
Manyeresa alisema pia itawajengea wananchi uhimilivu na ustahilimivu kwa masuala ya mabadiliko ya tabia ya nchi na wanaamini kwamba yana athari kubwa kwa jamii na yanawalenga sana wanawake.

Alisema kwa sababu mwanamke ndio wanakwenda kutafuta kuni na maji na usalama wa chakula nyumbani ukiwa dhaifuna kukiwa hakuna chakula watoto wanakwenda kumuambiwa mama.
MBUNGE UMMY AZINDUA LIGI YA WILAYA YA MPIRA WA MIGUU (TDFA ODO UMMY CUP),AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO
michezo
* Akabidhi seti za jezi 27 na mipira 31.
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu tarehe 17/11/2024 amezindua ligi ya mpira wa miguu inayosimamiwa na chama cha mpira wa miguu wilaya ya Tanga (TDFA) iliopewa jina la TDFA ODO UMMY CUP 2024/25.
Ligi hiyo inayoshirikisha Vilabu 27 vya Tanga Mjini itajumuisha jumla ya michezo 98 itakayochezwa katka viwanja vya Lamore Jijini Tanga
Sambamba na kutoa seti za jezi 27 na mipira 31, Mhe Ummy ataendelea kutoa pesa za uendeshaji wa ligi hiyo kwa michezo yote 98 na kuahidi zawadi nono kwa washindi wa 4 wa TDFA Odo Ummy Cup ambao pia watakwenda kucheza Ligi ya Mkoa.
Akiongea kwa niaba ya katibu mkuu TDFA ,katibu msaidizi Salimu Kalosi amempongeza Mhe Ummy na kusaema toka ligi hiyo ianzishwe hawajawahi kupata udhamini wa aina yoyote. Amemshukuru Mhe kwa kuweka historia Tanga Mjini na pia kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono michezo hususani Mpira wa Miguu Tanga Mjini.
Ufunguzi huo ulihudhuriwa na vilabu vyote 27 kutoka kila Kata, Viongozi wa CCM na serikali pamoja na wananchi na mashabiki wa mpira wa miguu.
Imetolewa na;
Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Tanga Mjini
18/11/2024.
WACHEZAJI WA MSD WANAOSHIRIKI MICHEZO YA SHIMUTA 2024 WAAGWA
michezoWachezaji wa Bohari ya Dawa (MSD) watakaoshiriki kwenye mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma,Taasisi na Makampuni Binafsi (SHIMUTA) mwaka 2024 jijiniTanga, leo Ijumaa tarehe 8 Novemba 2024 wameagwa na Menejimenti ya MSD na kuanza safari ya kuelekea kwenye mashindano hayo.
ZANZIBAR YAJIDHATITI KUJENGA MIUNDOMBINU YA MICHEZO
habari michezoNa. Mwandishi Wetu Zanzibar, Zanzibar.
MAKAMU wa Pili wa Rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla amesema kuwa, Serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya ya michezo Visiwani Zanzibar na kuboresha vivutio vya Utalii ili kuweza kuitangaza Zanzibar kimataifa na kuwavutia wanamichezo maarufu Duniani.
Ameyasema hayo kwa niaba ya Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi wakati wa kukabidhi zawadi kwa washiriki wa Tigo/Zantel Zanzibar International Marathon yaliyofanyika katika viwanja vya Forodhani jijini Zanzibar.
Amesema kuwa serikali ipo katika hatua ya kuimarisha miundombinu ya michezo kwa kuanza na ujenzi wa Uwanja mkubwa utatumika katika mashindano ya Afcon 2027 pamoja na kuvifanyia ukarabati mkubwa viwanja vya New Amani Complex na Uwanja wa Gombani Stadium Pemba.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais ametumia fursa kwa Kuwataka wanamichezo na wananchi kwa ujumla kuendelea kulipa kodi kwa hiari kwa kudai risiti wanaponunua bidhaa na kwa upande wa wafanyabiashara kutoa risiti wanapofanya mauzo jambo litakalosaidia kuziba myanya ya upotevu wa mapato ya Serikali na kuweza kupiga hatua kimaendeleo.
Mapema Mdhamini wa Zanzibar International Marathon Afisa Mkuu wa Biashara Tigo Zantel Isack Nchunda amesema kuwa antaendelea kudhamini mashindano mengine ili kuiunga mkono serikali ya awamu ya Nane ( 8 ) sambamba na kuviendeleza vipaji vilivyopo nchini kupitia michezo mbali mbali.