MBUNGE UMMY AZINDUA LIGI YA WILAYA YA MPIRA WA MIGUU (TDFA ODO UMMY CUP),AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO

November 18, 2024

 


* Akabidhi seti za jezi 27 na mipira 31.

* Mbunge Ummy kudhamini michezo yote 98. TDFA yasema ndio mara ya kwanza kupata Udhamini wa  Ligi ya Wilaya ianzishwe.

Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe Ummy Mwalimu tarehe 17/11/2024 amezindua ligi ya mpira wa miguu inayosimamiwa na chama cha mpira wa miguu wilaya ya Tanga (TDFA) iliopewa jina la TDFA ODO UMMY CUP 2024/25.

Ligi hiyo inayoshirikisha Vilabu 27 vya Tanga Mjini itajumuisha jumla ya michezo 98 itakayochezwa katka viwanja vya Lamore Jijini Tanga

Sambamba na kutoa seti za jezi 27 na mipira 31, Mhe Ummy ataendelea kutoa pesa za uendeshaji wa ligi hiyo kwa michezo yote 98 na kuahidi zawadi nono kwa washindi wa 4 wa TDFA Odo Ummy Cup ambao pia watakwenda kucheza Ligi ya Mkoa.

Akiongea kwa niaba ya katibu mkuu TDFA ,katibu msaidizi  Salimu Kalosi amempongeza Mhe Ummy na kusaema toka ligi hiyo ianzishwe hawajawahi kupata udhamini wa aina yoyote. Amemshukuru Mhe kwa kuweka historia Tanga Mjini na pia kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono michezo hususani Mpira wa Miguu Tanga Mjini.

Ufunguzi huo ulihudhuriwa na vilabu vyote 27 kutoka kila Kata, Viongozi wa CCM na serikali pamoja na wananchi na mashabiki wa mpira wa miguu.

Imetolewa na;
Ofisi ya Mbunge, Jimbo la Tanga Mjini
18/11/2024. 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »