Showing posts with label habari. Show all posts
Showing posts with label habari. Show all posts

NGORONGORO NA TANAPA WAPANUA WIGO WA KUNADI UTALII SOKO LA ULAYA

October 07, 2025 Add Comment

 Na Mwandishi Wetu, Barcelona – Hispania

Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) wameendeleza jitihada za kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia ushiriki wao katika maonesho ya utalii (Tourism Road Show) yanayofanyika nchini Hispania.

Onesho hilo lililoandaliwa na kampuni ya usimamizi wa safari (DMC) yenye makao makuu yake nchini Tanzania, (Tanganyika Expeditors) na kufanyika jijini Barecelona Oktoba 06, 2025 , limewaleta pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya utalii wakiwemo mawakala wa safari za kitalii pamoja na wawekezaji kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya jiji hilo. 

Kupitia ushiriki huo, NGORONGORO na TANAPA zimepata fursa kutoa taarifa muhimu za kuwasaidia mawakala wa usafiri kuandaa safari kwa wageni wanaotaka kutembelea Tanzania kujionea vivutio mbalimbali vinavyopatikana hifadhi ya  Ngorongoro na Hifadhi za taifa kama vile Serengeti, Manyara, Tarangire na maeneo mengine ya kipekee yanayosimamiwa na taasisi hizo.

Mbali na NCAA na TANAPA, washiriki wengine kutoka Tanzania ni pamoja na Miracle Experience -Tanzania, Auram Treks, Karafuu Beach Resort and Spa na Malia Hotels International.

Maonesho hayo ya Tourism Road Show yaliyoanza leo tarehe 6 Oktoba yataendelea kufanyika katika majiji mengine ya Hispania, ikiwemo Madrid na Seville ambapo yanatajiwa kuhitimishwa tarehe 8 Oktoba, 2025.






TTCL YASEMA "HAKUNA LISILOWΕΖΕΚΑΝA" ΚΑΤΙΚΑ KUTOA HUDUMA BORA

October 06, 2025 Add Comment


Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limezindua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka 2025, likiahidi kuendelea kuboresha huduma zake kwa ubunifu, kasi na ufanisi ili kukidhi mahitaji ya Watanzania na wateja wake wa kimataifa.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa wiki hiyo, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa TTCL, Bi. Anita Moshi, amesema maadhimisho hayo ni sehemu ya kujitathmini na kuimarisha uhusiano kati ya shirika hilo na wateja wake.

“Wiki hii inatukumbusha wajibu wetu wa msingi wa kumweka mteja mbele kama kiini cha mafanikio ya TTCL. Tunajitathmini, tunasikiliza, na tunajifunza kutoka kwa wateja wetu,” amesema Bi. Moshi.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja hufanyika duniani kote kila mwaka wiki ya kwanza ya Oktoba. Kwa mwaka huu, TTCL inasherehekea kuanzia Oktoba 6 hadi 10, 2025 chini ya kaulimbiu isemayo “Mission: Possible.”

Bi. Moshi amesema kaulimbiu hiyo imechaguliwa kuonyesha dhamira ya TTCL ya kuona kila changamoto kama fursa ya kuboresha huduma na kutafuta suluhisho la kudumu kwa manufaa ya wateja.

“Tutakuwa wabunifu, wenye bidii na maono. Kila mmoja wetu atakuwa sehemu ya suluhisho, na kwa pamoja tutahakikisha kila mteja anathaminiwa na kuhudumiwa kwa ubora wa hali ya juu,” amesisitiza.

Amesema TTCL imeendelea kutekeleza Mpango Mkakati wa kuboresha miundombinu ya mawasiliano nchini, ikiwa ni pamoja na kueneza Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hadi kufikia wilaya zote za Tanzania, pamoja na ujenzi wa minara 1,400 vijijini ili kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma za mawasiliano bila vikwazo.

Aidha, amesema kupitia huduma ya “Faiba Mlangoni Kwako”, TTCL inaendelea kuwapatia Watanzania huduma ya intaneti ya kasi na uhakika inayokidhi viwango vya kimataifa.

Bi. Moshi ameongeza kuwa TTCL itaendelea kuwekeza katika teknolojia bunifu, kuboresha mifumo ya huduma kwa wateja na kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma bora popote walipo.

Amewahimiza wateja waendelee kutumia Kituo cha Huduma kwa Wateja kinachofanya kazi saa 24, pamoja na mitandao ya kijamii na maduka ya TTCL nchini kote, kupata ushauri na taarifa muhimu.

“Tutaendelea kuwa karibu na wateja wetu, kuwaheshimu, na kuhakikisha wanapata huduma bora zenye ufanisi na thamani,” amesema.

Bi. Moshi amewashukuru wateja wote walioliweka TTCL kama chaguo lao la mawasiliano kwa miaka mingi na kuwataka waendelee kushirikiana na shirika hilo katika safari ya maendeleo ya kidijitali.

“Wateja wetu ndiyo msingi wa mafanikio yetu. Tutaendelea kuwa bega kwa bega nao kufanikisha azma yetu ya pamoja — Mission: Possible,” alisisitiza kabla ya kutangaza rasmi uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja ya TTCL kwa mwaka 2025.







WANANCHI WA IYAGABUYA GA-BUSEGA WAASWA KUFUATA SHERIA ZA UHIFADHI WANYAMAPORI

October 06, 2025 Add Comment



Na Mwandishi Wetu, Simiyu


Serikali imewaasa wananchi wa Kijiji cha Iyagabuyaga, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu kufuata sheria, kanuni na taratibu za uhifadhi wa wanyamapori ili kuepuka migogoro na Serikali pamoja na kuendeleza shughuli za uhifadhi endelevu nchini. 


 Afisa Wanyamapori Mkuu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Nassoro Wawa ameyasema hayo Oktoba 6, 2025 katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo kwa lengo la kutoa elimu ya uhifadhi na namna ya kukabiliana na changamoto za wanyamapori wakali na waharibifu, kufuatia tatizo la fisi lililokithiri katika eneo hilo.

Katika utoaji elimu hiyo unaofanywa na Timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, TAWA, na Maafisa Wanyamapori wa Halmashauri mkoani humo, Afisa huyo amesema Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori,  inasema kuwa mnyama ni nyara ya Serikali, na ukikamatwa huna kibali ni kosa la uhujumu uchumi."

Amesema Serikali imeweka mazingira rafiki kwa wananchi kushiriki katika shughuli za uhifadhi kisheria, ikiwemo kuanzisha bucha za wanyamapori, bustani, mashamba na ranchi za wanyamapori, hatua inayolenga kuchochea maendeleo na kuongeza kipato kwa wananchi.

“Sheria hizi zimekuja kumuwezesha mwananchi kunufaika na rasilimali za wanyamapori nchini ambazo ziruhusu mwananchi,  kikundi, kijiji kuanzisha bucha ya nyamapori, bustani, shamba na ranchi za wanyamapori ili kuinua kipato na kuleta maendeleo tunayoyataka,” amesisitiza.


Kwa upande wake, Afisa Uhifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA),  Lusato Masinde, amebainisha kuwa wananchi wanaruhusiwa kumuua mnyamapori anapothibitishwa kuwa tishio kwa maisha au mali, lakini kwa sharti la kutoa taarifa mara moja kwa viongozi wa Serikali.

 “Kama mnyamapori atahatarisha maisha au mali zako, unaweza kumuua lakini lazima utoe taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji, Mtendaji au Maafisa Wanyamapori. Nyara hizo ni mali ya Serikali na lazima zikabidhiwe sehemu husika,” ameeleza  Masinde.

Aidha, ameonya kuwa mtu yeyote atakayemuua mnyamapori bila kutoa taarifa kwa mamlaka husika atakuwa ametenda kosa na kufuatana na sheria atachukuliwa hatua kali za kisheria, ikiwemo kufunguliwa mashitaka ya uhujumu uchumi na akithibitika atahukumiwa kifungo.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Iyagabuyaga, Bw. Bahati Masaga, amesema changamoto ya fisi imekuwa kubwa kijijini hapo, na Serikali ilifanikiwa kuwaua fisi 17 hivi karibuni.


Ameishukuru Serikali kwa kutoa elimu ya kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu na kuahidi wananchi kuendelea kushirikiana na mamlaka husika katika kutatua tatizo hilo na kuwaomba waachane na imani potofu za kishirikina za kufuga fisi. 


&&&

TANZANIA YAIPONGEZA NORWAY KWA KUENDELEA KUUNGA MKONO MAENDELEO

October 05, 2025 Add Comment

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, ameipongeza Serikali ya Ufalme wa Norway kwa mchango wake mkubwa katika kuunga mkono juhudi za maendeleo ya Tanzania katika sekta za nishati, elimu, kilimo, na usimamizi wa fedha za umma.


Akizungumza kando ya Mkutano wa 22 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na nchi za Nordic uliofanyika mjini Victoria Falls, Zimbabwe, tarehe 2–3 Oktoba 2025, Mhe. Kombo alisema kuwa Norway imekuwa mshirika wa mfano katika kusaidia utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Ajenda ya 2030 kupitia miradi mbalimbali ya kimkakati nchini.

Mhe. Kombo alisema tangu mwaka 2010, Serikali ya Norway imechangia zaidi ya kronor bilioni 1.1, sawa na shilingi bilioni 300, kusaidia sekta muhimu zikiwemo nishati vijijini, elimu, mafuta na gesi, mabadiliko ya tabianchi, na usimamizi wa misitu. Alisisitiza kuwa msaada huo umechangia kuboresha huduma na kukuza uchumi wa wananchi wa Tanzania.

“Serikali ya Tanzania inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Norway katika kusaidia miradi ya maendeleo nchini, hususan katika nishati vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), uwezeshaji wa wanawake wahandisi, na uwekezaji wa kampuni ya Equinor katika gesi asilia,” alisema Mhe. Kombo.


Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Mhe. Espen Barth Eide, alieleza kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kukuza teknolojia ya nishati safi, elimu bora, na uwekezaji unaolenga kukuza uchumi wa kijani. Alisema Norway inaamini katika ushirikiano wa muda mrefu unaojengwa katika misingi ya uwazi, usawa na maendeleo endelevu.

Mhe. Kombo alihitimisha kwa kusema kuwa Tanzania itaendelea kudumisha uhusiano wa kihistoria na Norway, huku ikiahidi kuweka mazingira bora ya uwekezaji na ushirikiano wa kimaendeleo kwa manufaa ya wananchi wa mataifa yote mawili.

WAKILI JUDITH KAPINGA AWAAHIDI WANANCHI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA KIMAENDELEO

October 05, 2025 Add Comment

 


🗓️ *05.10.2025* 


📍 *Mbinga-Ruvuma🇹🇿* 


📌 *Ndugu.Kapinga awaasa Wananchi wa Kata ya linda kupiga Kura Oktoba 29*


📌 *Ndugu.Kapinga aeleza Ufanisi wa Ilani ya Uchaguzi 2020/2025 na Ilani ya Uchaguzi 2025/2030*


📌 *Ndugu.Kapinga awaombea Kura Mgombea Urais,Mbunge na Diwani kwa Wananchi wa Kata ya Linda*


➡️Mgombea Ubunge Jimbo la Mbinga Vijijini kupitia tiketi ya CCM *Wakili.Ndugu.Judith Kapinga* leo tarehe *05 Oktoba,2025* ameendelea na Ziara yake ya Kampeni ya kusaka Kura za CCM katika Kata ya Linda✍️.

➡️ *Ndugu.Judith Kapinga* amezungumza na Wananchi wa Vijiji vya Ndembo,Liombo,Ulolela na Lukiti.Mgombea huyo *Ndugu.Judith Kapinga* ameambatana na Timu ya Kampeni ya Jimbo la Mbinga Vijijini inayoongozwa na Mwenyekiti wa Timu ya Kampeni Jimbo la Mbinga Vijijini ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Mbinga, *Ndugu.Johnbosco Mkandawile✍️*



➡️Katika Ziara hiyo, *Ndugu.Judith Kapinga* ameeleza Ufanisi wa Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka *2020-2025* namna Kata ya Linda ilivonufaika lakini pia akaeleza Maendeleo yatakayofanyika kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka *2025-2030* ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Utekelezaji wa Maendeleo.Mgombea, *Ndugu.Kapinga* amepokea Kero za Kimaendeleo katika Vijiji hivyo na kuwaomba Wananchi kuwa atakwenda kuzishughulikia iwapo atachaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo,aidha *Ndugu.Judith Kapinga* amewaambia Wananchi kuwa Maendeleo ni Mchakato hivyo wawe Wavumilivu wakati Serikali ikiendelea kushughulikia ✍️

➡️ *Ndugu.Kapinga* amewaombea Kura kwa Wananchi,Mgombea Urais wa Tanzania, *Ndugu.Dkt.Samia Suluhu Hassan* ,Mgombea Mwenza, *Ndugu,Balozi,Dkt.Emmanuel Nchimbi,* Mgombea Ubunge yeye mwenyewe, *Ndugu.Judith Kapinga* na Mgombea Udiwani wa Kata ya Linda, *Ndugu.Desderius Haule.Ndugu.Kapinga* amewaasa Wananchi wa Kata ya Linda kujitokeza kwa wingi kupiga Kura *Oktoba 29*✍️



         *Imetolewa na Ofisi ya Mgombea Ubunge Jimbo la  Mbinga Vijijini,Leo tarehe 05.10.2025*