ZAIDI YA WANANCHI 9,450 KUNUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI WILAYA YA KOROGWE
habariZAIDI ya Wananchi 9,450 wa wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga wanatarajiwa kuondokana na changamoto ya upatkanaji wa maji baada ya Serikali kuzindua mradi wa Kitaifa wa Ujenzi wa Visima 900 ambao unalenga kutatua changamoto hiyo.
Kati ya visima hiyo Mkoa wa Tanga watapata visima 53 ambavyo vitajengwa kila jimbo
Akizungumza mradi huo katika Kijiji cha Makorora wilaya Korogwe Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian alisema kwamba visima 8 vimejengwa na kati ya hivyo vitano vimejengwa katika Jimbo la Korogwe Vijiji na Vitatu Korogwe mjini.
Alisema kwamba hatua hiyo ni juhudi za Serikali za kuhakikisha wana watua ndoo kichwani wakina mama hapa nchini kwa kuwekwa huduma hiyo karibu na maeneo yao ili kuwaondolea adha ambazo walikuwa wanakumbana nazo awali.
“Leo hii tumekuja kushuhudia katika jimbo la Korogwe Visima vilivyochimbwa na hivyo yote ni kuhakikisha tunamtua Ndoo kichwani Mama kama ilivyo azma ya Rais wetu Dkt Samia Suluhu tumefanya hivyo kuonyesha maji yamefika kwa wananchi”Alisema
Awali akizungumza Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Lugongo alisema kwamba wataendelela kuboresha huduma za maji katika maeneo ya vijiji kwa kuendeleza miradi ya maji kila eneo ambalo halijaunganishwa na huduma hiyo
Alisema huduma hiyo iwafikie ndani ya muda mfupi ili waweze kuondokana na adha ya kufuata maji umbali mrefu na hivyo kuwawezesha kushiriki kwenye shughuli nyengine za maendeleo.
Lengo la Serikali ni kuwapatia maji wananchi kwa asilimia 85 vijiji na aslimia 95 maeneo ya mijini
MARA WARIDHISHWA UTEKELEZAJI MIRADI YA REA
habari📌 Wamshukuru Rais Samia kwa kupunguza gharama za umeme
📌 Elimu kuhusu matumizi bora ya nishati yatolewa
📌 Watakiwa kuchangamkia fursa ya kuunganisha umeme
Wananchi mkoani Mara wamesisitiza kuridhishwa na utekelezaji miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), inayotekelezwa nchini kwa lengo la kuwapatia umeme wa gharama nafuu, na wameipongeza Serikali kwa kuwafikishia miradi hiyo muhimu yenye faida kwa uchumi wa Taifa.
Pongezi hizo zimetolewa na wananchi kwa Wataalam wa REA waliofika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kutumia fursa ya miradi ya REA inayotekelezwa katika Kata ya Kwangwa wilaya ya Musoma mkoani Mara.
Aidha, wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia fedha REA kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya umeme mkoani humo.
Awali Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka REA, Abdulrazack Mkomij ametoa elimu kwa umma kuhusu gharama za kuunganisha umeme, matumizi bora ya nishati, kuhamasisha kuunganisha umeme, tahadhari za umeme na elimu kuhusu utunzaji wa miundombinu ya umeme.
Naye, Mhandisi wa Miradi ya REA mkoa wa Mara, Omary Gwillah, amesema kuwa REA inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya umeme mkoani humo ili wananchi wafanye shughuli zao kwa tija.
Kwa upande wake, Mtendaji wa Kata ya Kwangwa, Bwiso Kinanda, ameishukuru Serikali kwa kupunguza gharama za uvutaji umeme. Amewataka wananchi kutumia fursa hiyo ya uvutaji wa umeme.
Vile vile, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kwangwa B, Maxmilian Kunju akizungumza kwa niaba ya wananchi ameiomba REA kuendelea kufikisha umeme kwenye maeneo mengine mkoani humo ili wananchi wa Musoma wapate nishati ya umeme.
TANESCO YAANZA KAMPENI YA KUTOA ELIMU YA USALAMA KWENYE MATUMIZI YA UMEME MIKOA YA KANDA YA ZIWA
habari magazeti📌Kampeni inalenga kuelimisha watoto kuzingatia usalama kwanza watumiapo umeme.
📌Itasaidia Kupunguza athari na ajali zitokanazo na majanga ya umeme kwenye Mikoa hiyo.
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Machi 27 limeanza kampeni maalumu ya kuelimisha juu ya kuzingatia usalama kwanza kwenye matumizi ya Umeme kwa Makundi ya watoto katika shule mbalimbali za msingi zilizopo kwenye mikoa ya Mara, Kagera, Mwanza, Geita na Simiyu.
Kampeni hiyo inayoitwa " Zingatia Usalama Kwanza Utumiapo Umeme" inalenga kuwafikia wanafunzi wa shule za msingi na kuwapa elimu inayowawezesha kugundua vihatarishi vinavyoweza kusababisha ajali zinazotokana na majanga ya umeme na kuepuka athari zitokanazo na majanga hayo.
Akizungumza katika moja ya Shule zilizotembelewa Kaimu Meneja Masoko kutoka TANESCO Bwana Sylvester Matiku amesema elimu hiyo ni muhimu kuwalinda watoto na majanga ya umeme kutokana na kuwa kati ya makundi yanayopata athari zaidi na ajali za umeme.
''Shirika limeona lianze kampeni hii hasa kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na hivi karibuni kuwa na matukio ya ajali zitokanazo na umeme zinazoathiri zaidi watoto na hivyo tukaona tuje kuwaelimisha ili kusaidia kupunguza na kuondoa madhara ya ajali zitokanazo na umeme''.
Wanafunzi hao wamepatiwa elimu kuhusu Matumizi Sahihi ya Umeme ili kuokoa gharama pamoja na kuitambulisha namba mpya ya ya huduma kwa wateja bila malipo ya Mchongo 180.
Katika kampeni hiyo Wanafunzi katika shule mbalimbali wamepata fursa ya kuhoji maswali kuhusu umeme na athari za umeme na jinsi ya kumsaidia muathirika wa ajali za umeme.
Wanafunzi hao wameahidi kufikisha elimu waliyoipata kuhusu Umeme na Usalama katika Kampeni ya hiyo kwa familia zao, ndugu, jamaa na marafiki na wameomba elimu hiyo pia ifikishwe kwa Wanafunzi Wenye Mahitaji Maalum.
Kampeni hii muhimu inaendelea kwenye mikoa yote Kwenye Kanda ya Ziwa.
KAMPUNI YA SUNKING YAUNGA MKONO AGENDA YA RAIS SAMIA
habari