Na Oscar Assenga,TANGA
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa)
imepongezwa kwa kiongozi wa mbio wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ismail Ali
Ussi kwa kutekeleza kwa vitendo agizo la Rais Dkt Samia Suluhu la ufungaji wa
mita za maji za malipo kabla kwa wananchi lengo likiwa kuboresha utoaji wa
huduma
Pongezi hizo zimetolewa leo na Kiongozi wa Mbio mara baada ya
kutembelea na kukagua mradi wa Ufungaji wa Dira za Malipo kabla katika eneo la
Mwakidila kata ya Tangasisi Jijini Tanga baada ya kupokea taarifa ya mradi na kujionea hali ya halisi ya utekelezaji wake.
Alisema kwamba amewapongeza kutokana na kwamba mamlaka hiyo kuwa
wasikivu na kutekeleza agizo la MRais kwa
mradi huo wa kimkakati unaoenda kuondosha changamoto ya muda mrefu
ambayo walikuwa wakiipata wananchi ya malalamiko ya bili za maji.
Alisema kwamba mfumo huo sasa unaenda kuondosha lawama kwa
viongozi kwani wananchi wanaenda kupata maji kulingana na uwezo wao hivyo
kutokana na hilo wamehaidi kwenda kuwa mabalozi waziri kwa kuwasemea juu ya
usimamizi wao mzuri wa mfumo huo kwa sababu unaenda kuwasaidia wananchi hivyo
tunawashukuru na kuwapongeza sana kwa kazi hii nzuri.
Awali akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa Mradi huu kwa kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025,Meneja wa Ankara na Makusanyo wa Tanga Uwasa Francis
Barabara alisema kwamba mradi huo ulianza kutekelezwa mwezi Julai mwaka jana na una thamani ya Shilingi za Kitanzania
Bilioni 1.87 na unatekelezwa kwa fedha za Serikali Kuu kupitia programu ya
IFF-OBA na Mfuko wa Maji wa Taifa.
Francis alisema kwamba utekelezaji wa mradi huo kwa sasa umefikia
asilimia 55.05 kwa ufungaji wa dira 2,202 kati ya dira 4,000.
Aidha alisema utekelezaji wa mradi huu utaongeza Ufanisi wa
ukusanyaji wa mapato na kupunguza madeni ya wateja, udhibiti wa upotevu wa maji,
uimarishaji wa matumizi sahihi ya maji kwa wateja na hivyo kupunguza malalamiko
ya bili za maji.
Akizungumza wakati mara baada ya Mwenge wa Uhuru kukagua na
kutembelea mradi huo,Mwenyekiti wa Bodi
ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo alisema maboresho kupitia mradi wa
hati fungani ambao upo kwenye hatua ya utekelezaji una thamani ya Sh.Bilioni 53.
Alisema kwamba katika mradi huo wamedhamiria kuboresha
miundombiniu kwenye chanzo cha maji bwawa la mabayani ambalo lilijengwa muda mrefu
1978 hivyo kutokufanyiwa ukarabati hivyo wameona walifanyie ukarabati ili
liweze kuendana na uhitaji wa maji kwenye mji wa Tanga,Pangani na Mkinga.
Aliongeza kwamba hivyo wanarekebisha mtambo kwenye bwawa na
katika pampu ambazo zinapeleka maji kwenye mtambo wa kutibu maji sehemu hiyo ikiwemo kurekebisha kuweka
mabomba mapya na kutoka eneo hilo kupelekea mjini kuna bomba kubwa linalazwa .
Mwenyekiti huyo alisema kwamba hatua nyengine ni kusambaza maji kwenye
mji wa Tanga na mabomba yaliyopo ni ya zamani yamechakaa na kama watafanikiwa presha itakuwa kubwa na
mabomba ya zamani yanashindwa kuhimili na watarekebisha ili kuweza kuhimili na
mradi huo mpaka Octaba mwaka huu utakuwa wamemaliza marekebishi na utaanza
kufanya kazi.
Akizungumza mita za Luku, Dkt Fungo alisema kwamba matarajio yao
ni kuhakikisha wananchi wanaunganishwa na nazo kwa wale ambao hawajafikiwa
ambapo alisema kabla ya kufunga mita za luku kulikuwa na malalamiki sana kwa
wateja kuona kama wanabambikiziwa bili kitu ambacho hakiwezekana.
Alisema lakini kwa kuondoa shida hiyo kwa wananchi na Rais alitoa maelekezo kuona njia bora ya kuweza kurekebisha dosari zilizojitokeza na hivyo njia bora wakaona ni mita za luku na walifanya majaribio kwa miaka miwili na sasa wamefikia mita ambazo zinaweza kukudhi mahitaji.
“Tumeanzaa na kuzifungwa kwa wateja wetu na na tulianza na mita 4000 na mpaka sasa tumefikia asilimia 60 wamefunga mita 2200 na tunatarajia kuzimaliza kwa kuwafungia watu wenye uhitaji na wale waliokuwa na madeni na muda mfupi tutakuwa tumezimaliza kwa wenye madeni”Alisema
Awali ya pili mradi wa Mradi wa Hat fungani utakuwa na mita
10,000 kwa hiyo wanataraji kuwafikia wananchi kwa wananchi wengi Tanga kutokana
na mahitaji ni mengi kutokana wenye uhitaji wa kubadilishiwa mita za luku wana
wateja kkaribia 50,000 bado wanaendeleaa kuomba na wanatarajiwa kufikia mpaka
75,000 na ubadilishaji wa mita utakuwa ni urtarbu wa kudumu wataweka za luku.
MWISHO.
EmoticonEmoticon