Showing posts with label afya. Show all posts
Showing posts with label afya. Show all posts

TRILIONI 6.7 YAFANYA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA AFYA

November 08, 2024 Add Comment

 Na WAF - Dodoma


Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema Shilingi Trilioni 6.7 zilizotolewa na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan zimechangia kuleta mageuzi makubwa ya upatikani wa huduma bora za afya ikiwemo matibabu ya kibingwa nchini.

Dkt. Mollel amesema hayo wakati akichangia hoja kwenye Kamati ya Mipango na Uwekezaji Novemba 07, 2024 bungeni jijini Dodoma.

“Uwekezaji wa kiasi cha Shilingi Trilioni 6.7 umeleta mabadiliko makubwa katika huduma za afya, hali ya ubora wa huduma za afya umeendelea kuimarika nchini na hospitali zote za rufaa sasa zimepata vifaa vya kisasa, ikiwemo CT Scan, huku hospitali za kanda zikifungwa mashine ya MRI, hatua inayomuweka Rais Samia katika rekodi za kihistoria,” amesema Dkt. Mollel.

Dkt. Mollel amesema kiwango cha vifo vya kina mama kimepungua kutoka 556 hadi 104, akieleza kuwa mafanikio hayo yanaonesha upunguzaji wa asilimia 81.2 katika vifo vya uzazi.

Ameongeza kuwa Serikali imepunguza vifo vya wagonjwa wa kansa kwa asilimia 78, kutokana na upatikanaji wa matibabu ya kisasa ndani ya nchi.

Dkt. Mollel ameeleza kuwa kwa sasa Watanzania wengi hawalazimiki kwenda nje ya nchi kutibiwa, tofauti na ilivyokuwa kipindi cha nyuma ambapo mgonjwa aliyetakiwa kwenda India kupata matibabu alihitaji zaidi ya milioni 100, lakini sasa gharama zimepungua hadi milioni 10, huku huduma hizo zikitolewa ndani ya Tanzania. Kutokana na maboresho haya, rufaa za matibabu nje ya nchi zimepungua kwa asilimia 97.

Aidha, Naibu Waziri huyo amesema kuwa vifaa vya kisasa kama PET CT Scan vimewekwa ili kugundua kansa mapema, hata ile inayoweza kuibuka miaka 10 ijayo. Mafanikio haya yamewezesha wagonjwa 10,931 kutoka nje ya Tanzania kufika nchini kwa ajili ya matibabu, jambo linalodhihirisha uwekezaji mzuri uliofanywa na Rais Dkt. Samia katika sekta ya afya.




TPDC YACHANGIA MILIONI 50 KUSAIDIA WATOTO WENYE UHITAJI WA MATIBABU JKCI

November 03, 2024 Add Comment
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limechangia kiasi cha shilingi milioni 50 kwa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa lengo la kusaidia watoto wenye uhitaji wa Matibabu ya moyo.

TPDC imechangia fedha hizo kwenye hafla ya uchangishaji fedha kusaidia watoto 1500 wenye matatizo ya moyo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo ni Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

Tukio hilo limefanyika jana tarehe 02.11.2024 , Johari Rotana Jijini Dar es salaam.




RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AONGOZA HARAMBEE KUCHANGIA GHARAMA ZA MATIBABU KWA WATOTO KUTOKA FAMILIA ZISIZO NA UWEZO WENYE UGONJWA WA MOYO

November 03, 2024 Add Comment

 

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zungu wakiingia ukumbini  katika harambee aliyoongoza kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku  jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na sehemu ya timu ya wataalamu iliyoongozwa na  Prof. David Mwakyusa (wa tatu toka kushoto nyuma), ambaye akiwa Waziri wa Afya, yeye Profesa Mohamed Janabi (hayupo pichani) na timu hiyo walitoa mchango mkubwa katika kuanzishwa kwa Taasisi ya JKCI mwaka 2015. 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zung na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jaffo  akitoa cheti cha shukurani kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya NMB kwa mchango wao wa shilingi bilioni moja katika harambee ya kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku  jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zung na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jaffo  akitoa cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Insurance Company Bw. wilson Mzava kwa mchango wao wa zaidi ya shilingi milioni 700 katika harambee ya kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku  jijini Dar es Salaam.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zung na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jaffo  akitoa cheti cha shukurani kwa mwakilishi wa taasisi ya kimataifa ya BAPS Charities tawi la Tanzania kwa mchango wake wa dola za Kimarekani laki nne (takriban shilingi 1,078,674,800) katika harambee ya kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku  jijini Dar es Salaam.

 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Naibu Spika Mhe. Mussa Hassan Zung na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Suleiman Jaffo  akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Albert Chalamila zawadi ya picha ya kuchora ikimuonesha akimpa pole mtoto wa kwanza kufanyiwa upasuaji wa moyo wakati huo huduma zikipatikana MOI  katika harambee ya kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku  jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya wadau waliohudhuria katika harambee aliyoongoza Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuchangia gharama za matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Johari Rotana Jumamosi usiku  jijini Dar es Salaam



Na Issa Michuzi

 Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa wito kwa taasisi na watu binafsi wenye nia njema kujitokeza na kuchangia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo ili kuwaondolea au kupunguza mateso yanayosababishwa na maradhi hayo.

 Dkt. Kikwete alitoa wito huo Jumamosi usiku wakati wa harambee aliyoongoza kuchangia gharama za matibabu ya watoto hao, iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Joihari Rotana, jijini Dar es Salaam.

 Rais Mstaafu, ambaye ni mlezi wa watoto wanaohitaji matibabu ya moyo, alieleza kuwa lengo kuu la harambee hiyo ni kuchangisha asilimia 30 ya gharama zilizobaki za matibabu, kwani asilimia 70 ya gharama hizo huchangiwa kila mwaka na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 "Naishukuru serikali kwa kuchangia asilimia 70 ya gharama zote za matibabu ya wagonjwa hao. Hata hivyo, asilimia 30 iliyobaki, ambayo familia ya mgonjwa inapaswa kuchangia, bado ni mzigo mzito kwa familia nyingi. Wanahitaji kusaidiwa," alisema.

 Alieleza kuwa kuna watoto 1,500 kutoka familia zisizo na uwezo ambao wamesajiliwa JKCI wakisubiri matibabu ya haraka ili kuokoa maisha yao. Bila matibabu hayo, watoto hawa wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupoteza maisha.

 "Nawashukuru sana wadau wote waliochangia katika harambee hii ambapo hadi sasa kiasi cha shilingi 2,718,525,000/= kimepatikana. Kiasi hiki kitawezesha kugharamia matibabu ya watoto 500 ambao wanahitaji huduma ya haraka," aliongeza Rais Mstaafu.

 Akitoa shukurani za pekee kwa Benki ya NMB kwa mchango wake wa shilingi bilioni moja, aliomba taasisi zingine ziige mfano huu si tu kwa kuwasaidia wagonjwa, bali pia kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kupunguza au kutatua tatizo hilo.

 Pia aliipongeza na kuishukuru taasisi ya kimataifa ya BAPS Charities tawi la Tanzania kwa mchango wake wa dola za Kimarekani laki nne (takriban shilingi 1,078,674,800), pamoja  na Benki ya CRDB kwa kuchangia zaidi ya shilingi milioni 700 katika vipindi tofauti huku ikiahidi kuendelea na zoezi hilo kila mwaka.

 Rais Mstaafu aliwashukuru pia wadau wote waliojitokeza kwenye hafla hiyo kwa kuchangia pesa na wengine kutoa ahadi, akiwaomba kila mmoja wao kuheshimu ahadi aliyotoa ili kufanikisha zoezi zima la kuwaokoa watoto hao wenye matatizo ya moyo.

 Dkt. Kikwete pia aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na ya Sita kwa kuendelea kuwekeza kwenye vifaa vya kisasa katika JKCI na kuleta madaktari bingwa, jambo ambalo limeiongezea uwezo JKCI wa kuhudumia Watanzania wenye maradhi ya moyo.

 Alitumia hafla hiyo pia kumtambulisha Prof. David Mwakyusa, ambaye alisema akiwa Waziri wa Afya, yeye na timu yake ya wataalamu aliyoiongoza walitoa mchango mkubwa katika kuanzishwa kwa Taasisi ya JKCI mwaka 2015.

 Mwenyekiti wa HTAF, Mhe. Mussa Hassan Zungu, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemshukuru Rais Mstaafu kwa kubuni na hatimaye kuanzisha Taasisi ya JKCI, ambayo kwa sasa ni ya tatu kwa ubora barani Afrika, ikifuatia kwa karibu taasisi kama hizo za Misri na Afrika Kusini.

 Mhe. Zungu alieleza kuwa uwepo wa JKCI umepunguza kwa kiwango kikubwa gharama za matibabu ya wagonjwa wa moyo, kwani uwepo wa taasisi hiyo umewezesha matibabu yaliyokuwa yakipatikana India na nchi zingine kwa gharama kubwa, sasa kupatikana hapa nchini na kwa ubora uleule wa huduma za nje.

 Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI katika risala yake alisema hivi sasa taasisi hiyo imefikisha uwezo wake wa kutoa huduma kwa kiwango cha asilimia 90, na kwamba ina madaktari bingwa wazawa 50 na wa kawaida zaidi ya 40 wanaotoa huduma za kisasa.

 Hivi karibuni, JKCI imepokea tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango mkubwa na wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024.

 Tuzo hiyo ilitolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akifungua kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kufanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

 Tuzo hiyo inatoa heshima kwa JKCI kwa hatua zake za kufanikisha malengo ya taasisi na kusaidia taasisi zingine kuweza kufikia mafanikio sawa katika utoaji wa matibabu ya moyo.

 Mafanikio haya yanaonesha kazi nzuri ya Taasisi hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita ambapo JKCI ilitoa huduma za upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua kwa wagonjwa 654, ambao hapo awali walihitajika kwenda nje ya nchi kwa matibabu.

 Kupitia upasuaji huo, JKCI imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 9.8 za Kitanzania kutokana na huduma hizi kupatikana ndani ya nchi.

 JKCI pia imezijengea uwezo nchi za jirani katika kutoa huduma na matibabu ya magonjwa ya moyo, ikiwemo Hospitali ya Moyo ya Zambia, Hospitali ya King Faisal ya Rwanda, Hospitali ya Queen Elizabeth ya Malawi, pamoja na hospitali mbalimbali za hapa nchini.


PANDENI MITI KWA MAZINGIRA BORA YA KUJISOMEA- WAZIRI MHAGAMA

October 08, 2024 Add Comment

 Na Linda Akyoo -Moshi


WAZIRI wa Afya Jenista Mhagama ameuagiza uongozi wa Shule ya Sekondari Dkt Asha Rose Migiro iliyopo Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro kuotesha miti katika shule hiyo ili wanafunzi wa shule hiyo wapate mazingira mazuri,Safi na bora ya kujisomea.

Ameyasema hayo leo tarehe 07 Oktoba,2024 kwenye ziara ya kutembelea Shule hiyo ambapo ameweza kukaguwa majengo mapya ya madarasa na mabweni ya kidato cha tano na chasita.

Aidha amsifu mradi huo wa madarasa pamoja na mabweni na kusema kuwa umekuwa mradi namba moja kati ya miradi yote niliyo itembelea".

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro Nurdin Babu, amesema l pamoja na Waziri Mhagama anashughulikia Afya lakini ametembelea miradi mingine kama vile Shule ambayo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi za maendeleo na kufafanua Sh.bilioni 915 zimepelekwa katika mkoa huo.

Awali Mkuu wa shule ya Dkt.Asha Rose Migiro ,Flaviana Sumawe ameishukuru serikali kwa kuongeza shule hiyo kwa kidato cha tano na chasita na kusema ukimwelimisha mwanamke umeelimisha Taifa zima.

Shule ya Sekondari ya Dkt Asha Rose Migiro ilianzishwa mwaka 2010 ikiwa na wanafunzi 361,shule ilipokea shilingi Milioni 429 kwaajili ya upanuzi wa kidato cha tano na chasita,huku lengo likiwa ni kutoa elimu kwa mtoto wa kike wa Kitanzania.


NHIF TANGA KUTUMIA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA KUSIKILIZA NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANACHAMA WAO

October 07, 2024 Add Comment



Na Oscar Assenga, TANGA.


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Tanga umesema kwamba watatumia wiki ya huduma kwa wateja kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wanachama wao wanaowahudumia.

Hayo yalibainishwa leo na Msimamizi wa Ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Fredrick Mtango wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kwamba wanatumia siku hiyo pia kuwahudumia wanachama wao ofisini kwao.

Alisema pia wanatarajia kupitia kwenye Hospitali zilizopo Tanga mjini kuonana na wateja wao na kusikiliza changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo ili kuweza namna ya kuzipatia ufumbuzi.

“Tunaamini itakuwa wiki njema itakayokuwa na manufaa kwa mfuko na wateja wao kwa ujumla lakini pia nisisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kujiunga na mpango wa bima ya afya kuweza kunufaika na huduma za matibabu “Alisema

Awali wakizungumza huduma za mfuko huo baadhi ya wanachama wao akiwemo Noel Mahundi ni Mwalimu Mstaafu kutoka wilaya ya Korogwe alisema huduma za bima ya afya ni nzuri kwa sababu zinawasaidia watu waliokuwa wamestaafu wanapata matibabu wanapokuwa wakiugua.

Alisema huduma zinazotolewa na nzuri kwa sababu zipo ambazo zimeongeka hasa baadhi ya dawa ambazo awali walikuwa hawawezi kuzipata lakini kwa sasa wakienda Hospitalini wanazipata.

Naye kwa upande wake Ailice Barua anashukuru huduma zao ni nzuri na ukienda hospitali unahudumiwa vizuri na upatikanaji wa dawa ni wa uhakika hivyo wasiopokuwa na bima wanapata shida .

Aliwashauri wananchi kuona umuhimu wa kujiunga na mpango wa bima ya afya ili kuweza kunufaika na huduma mbalimbali zikiwemo za matibabu bure pindi wanapokuwa wakiugua.



Mwisho.

VITUO VYA AFYA VITANO VIPYA VYAJENGWA WILAYA YA HAI

October 04, 2024 Add Comment

             


                  

Na WAF – Kilimanjaro

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi kwa kujenga vituo vya Afya Vitano katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro.

Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amesema hayo leo Oktoba 4, 2024 akiwa katika ziara ya siku Sita Mkoani Kilimanjaro ambao ameanza kwa kukagua na kuzindua miradi ya Sekta mbalimbali iliyotolewa fedha na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwemo Sekta ya Afya.

“Mkoa huu wa Kilimanjaro umepokea zaidi ya Bilioni 10 ili kutekeleza miradi ya Afya vilevile Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza milioni 150 kwa ajiri ya vifaa tiba vitakavyotumika katika kituo cha Afya Masama Kati.” Amesema Waziri Mhagama

Aidha, Waziri Mhagama ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa kukamilisha ununuzi wa vifaa tiba ili Zahanati ya Kimashuku ianze kufanya kazi ifikapo Oktoba 30 mwaka huu.

“Kwa kuwa Mhe. Rais Samia ameleta Milioni 100 ya umaliziaji wa Zahanati hii na Milioni 50 ya ununuzi wa vifaa tiba, jambo la kwanza naomba fedha ya vifaa ipelekwe Bohari ya Dawa haraka sana, nimachotaka kuona Zahanati hii upatikanaji wa dawa usiwe wa mashaka.” Amesema Waziri Mhagama

Waziri Mhagama ameukata uongozi huo kuhakikisha huduma za uzazi wa dharula kwa kina mama zinapatikana ikiwemo vitanda maalum vya kujifungulia ili wakina mama wapate eneo salama na zuri la kujifungua na kuwapunguzia adha wananchi ya kufuata huduma hizo mbali.

“Tunatamani Zahanati hii iwe mkombozi kwa akina mama, wazee, vijana na watoto wetu, nitoe wito kwa Halmashauri yetu kuhakikisha Zahanati yetu inasimamiwa vizuri na tunaamini Zahanati hii itaenda kutoa huduma zinzotakiwa.” Amesisitiza Waziri Mhagama

Mwisho, Waziri Mhagama amewataka wananchi wote wa Hai kwenda kujiandikisha kuboresha taariza kwenye tume ya uchaguzi ili kupata fursa ya kuwachagua viongozi wa Serikali za mitaa ambao wanaleta maendelea katika maeneo yao.