NEMC YAELEZA NAFASI YAKE KATIKA KONGAMANO LA 5 LA KIMATAIFA LA UCHUMI WA BULUU

September 08, 2026
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), katika Kongamano la 5 la Kimataifa la Uchumi wa Buluu, limejipambanua katika sekta ya mazingira kwa kusisitiza umuhimu wa matumizi endelevu ya rasilimali za bahari, mito, maziwa na maeneo ya pwani, sambamba na uhifadhi na usimamizi endelevu wa mazingira.

NEMC imeeleza kuwa hakuna Uchumi wa Buluu endelevu bila mazingira safi na salama, kwa kuwa mazingira yenye afya ni msingi wa rasilimali zinazotoa ajira, chakula, mapato na fursa za uwekezaji kwa kizazi cha sasa na kijacho.

Kupitia kaulimbiu “Powering Blue Initiatives for Sustainable Economic Growth in Africa,” NEMC imeendelea kutekeleza majukumu yake kupitia Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA), ukaguzi, ufuatiliaji wa uzingatiaji wa masharti ya mazingira na udhibiti wa uchafuzi.

Baraza pia limeonya kuwa uchafuzi wa bahari, taka za plastiki na uharibifu wa ikolojia ya pwani ni changamoto kwa Uchumi wa Buluu endelevu.

Kongamano hilo limefunguliwa rasmi leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi Hamad Yusuf Masauni, kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi.

NEMC imesisitiza kuwa uhifadhi wa mazingira si kikwazo cha Uchumi wa Buluu, bali ni msingi wa ukuaji wa uchumi wenye manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho

Share this

Related Posts

Latest
Previous
Next Post »