Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuletea mashindano ya Wazo Bunifu yanayolenga kupata suluhisho za kibunifu zitakazochangia kuboresha mfumo wa kodi nchini. Hii ni fursa yako ya kuwasilisha wazo lenye tija na kushindania zawadi ya hadi Shilingi Milioni 50.
Mawazo yatakayowasilishwa yanapaswa kulenga eneo moja au zaidi kati ya yafuatayo ; kupanua wigo wa kodi, kurahisisha ukadiriaji na ulipaji wa kodi kwa biashara ndogo ndogo, kuimarisha huduma za kodi za kidijitali, kupunguza gharama za ukusanyaji wa mapato, kutumia teknolojia za kisasa kama AI, Big Data na Blockchain katika usimamizi wa kodi, pamoja na kuboresha utatuzi wa migogoro ya kodi ili kuwa wa haraka, wazi na wenye kuaminika zaidi.
Kutuma Wazo lako ingia tovuti ya TRA, Bonyeza kitufe cha innovation portal fuata hatua zinazofuata, Mwisho wa kutuma wazo lako bunifu ni julai 31, 2026.
MWISHO WA SHINDANO HILI NI MWEZI HUU WA 7 NI HATARII

EmoticonEmoticon