NAIBU WAKILI MKUU WA SERIKALI ATEMBELEA MAONESHO SABASABA

July 08, 2026
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Bi. Alice Mtulo (aliyesimama katikati) akiwa pamoja na watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wakati wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo (aliyesimama kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Uratibu na Huduma za Kisheria wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Neema Ringo alipotembelea banda la Maonesho la Ofisi hiyo wakati wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye banda la Maonesho la Wizara ya Katiba na Sheria wakati wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akipokea maelezo kutoka kwa Mawakili wa Serikali wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania alipotembelea banda la Tume hiyo wakati wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akipokea Jarida la Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania kutoka kwa Mawakili wa Serikali wa Tume hiyo baada ya kutembelea banda la Maonesho la Tume hiyo wakati wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akipokea maelezo kutoka kwa Afisa wa Idara ya Uhamiaji Tanzania kuhusu namna Idara hiyo inavyofanya kazi wakati wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Usuluhishi wa Wizara ya Katiba na Sheria ndugu Felix Chakila kuhusu namna Wizara hiyo  inavyohudumia wananchi wakati wa   Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo (aliyeketi kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma, Mawasiliano, Tafiti na Nyaraka wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,
Bi. Monica Mnanka alipotembelea banda la Tume hiyo wakati wa Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.
Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akizungumza na viongozi wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) alipowasili kwenye viwanja vya Maonesho ya Kimataifa vya Mwalimu Nyerere kutembelea Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »